img

Leo siku ya walemavu duniani,Chama cha wasioona Manispaa Mtwara Mikindani waeleza changamoto zao

December 3, 2020

Na Faruku Ngonyani,Mtwara

Ikiwa leo tarehe 03 Disemba 2020 Dunia kwa ujmla inaadhimisha siku ya walemvu ambapo kwa Tanzania kitafa imefanyika Mkoani Dododma.
Katibu wa Chamacha watu wasioona Manispaa Mtwara Mikindani Ndg Saidi Mtanga amesema kuwa kwa upande wao siku hii wameipokea vyema sipokuwa kwa upande wao hawajafanya sherehe yeyoteIkia.
Lakini pia Ndg Saidi ameelezea changamoto wanazokutatazo wasioona ikiwa ni pamoja na tatizo la uchumi kuwa mdogo,mwamko mdogo wa wazazi wenye watoto walemavu kuwaruhusu watoto wao kwenda shule pamoja na gharama za masomo kwa kuwa shule wanazotakiwa kusoma zipo wilaya ya Masasi .
Aidha Saidi ameongeza kuwa na ni vyema kwa Halmashauri ya Manispaa Mtwara Mikindani wakawaangalia waleemavu hao juu ya mikopo kwani mashariti na vigezo vya kupata mikopo haswa 2% kwa walemavu kwa upande wao wanashindwa kufuata ili kuweza kuipata mikopo hiyo.
Nae mjumbe wa Chama cha wasioona Manispaa Mtwara Mikindani Ndg Abdurah Lisinge ametoa wito kwa Serikali kuitangza siku ya walemavu kama zilivyo siku zingine za matukio ili wananchi na walemavu wengine waweze kuijua na kuadhimisha pamoja.
Siku ya walemavu duniani huadhimishwa kila ifikapo tareh 03 Disemba kwa kila mwaka.
 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *