img

KMC FC kushuka dimbani kesho dhidi ya Dodoma jiji

December 3, 2020

Timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC kesho itashuka dimbani kumenyana na Timu ya Dododma Jiji mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, saa 10.00 jioni huku kikiwa na matumaini makubwa ya kupata matokeo mazuri katika mchezo huo.

Katika mchezo huo KMC FC ambao niwenyeji wamefanya mazoezi ya mwisho leo ikiwa ni katika kuhakikisha kwamba wanapata matokeo mazuri na hivyo kujiweka katika nafasi nzuri kwenye  msimamo wa Ligi kuu Soka Tanzania bara.

Kikosi hicho ambacho kinanolewa na makocha wa zawa ambao ni John Simkoko pamoja na Habibu Kondo hadi sasa kimefanya maandalizi ya kutosha kutokana na kuwa na muda mwingi katika mazoezi na hivyo wachezaji wote kwa nafasi yao wamejiandaa kuiwezesha Timu hiyo kupata matokeo mazuri.

Aidha wachezaji wa KMC FC wameonyesha kuwa na morali nzuri kuelekea katika mchezo huo kwakuwa wanahitaji ushindi mkubwa licha ya kwamba Timu ya Dodoma Jiji imekuwa ikipata matokeo mazuri katika michezo yake.

“Tunawafahamu wapinzani wetu kuwa ni wazuri, tunawafuatilia katika michezo yao, lakini pia hata tuna kiwango kizuri na bora kimchezo,na  ushindi kwenye mchezo huo upo ndani ya uwezo wetu, hivyo mashabiki na wapenzi wa KMC FC wategemee kupata burudani safi, sambamba na kuona Pira Spana, Pira Kodi, Pira Mapato  katika uwanja wetu wa nyumbani.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *