img

Iran yaweka sheria mpya ya kukuza uzalishaji wa nyuklia

December 3, 2020

Dakika 5 zilizopita

A satellite image shows Iran's Natanz nuclear facility in Isfahan, Iran, 21 October 2020

Maelezo ya picha,

Eneo la shuguli za kinyuklia-Natanz

Bunge la Iran limepitisha sheria ya kuwazuia wachunguzi wa Umoja wa Mataifa katika maeneo yao ya shughuli za kinyuklia na kuongeza uzalishaji wake wa Urani.

Sheria hiyo itaitaka serikali kurejelea urutubishaji wa urani kwa asilimia ishirini.

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema anapinga kupitishwa kwa sheria hiyo ambayo inakiuka makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2015 kati ya Iran na nchi zenye nguvu zaidi ulimwenguni ya kudhibiti mpango wa kinyuklia wa nchi hiyo kutokwenda zaidi ya asilimia 3.67 na kuongeza itahujumu diplomasia.

Bunge la Iran linataka wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wa kudhibiti silaha za kinyuklia kuzuiwa kuchunguza vitu vya kinyuklia na kuongeza uwezo wake wa kuzalisha urani katika kinu cha Natanz na Fordow iwapo vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran havitaondolewa katika kipindi cha miezi miwili ijayo.

Vikwazo hivyo vilivyolenga sekta ya mafuta na fedha ya Iran vilirejeshwa na nchi za magharibi baada ya Marekani kujiondoa kutoka makubaliano hayo ya kihistoria yaliyofikiwa 2015.

Iran's President Rouhani said his government did not agree with the Iranian parliament's draft bill to increase nuclear activities

Maelezo ya picha,

Rais Rouhani alisema serikali yake haikubaliani na ongezeko la gharama za shughuli za nuyklia

Hayo yanakuja baada ya mwanasayansi mwandamizi wa masuala ya nyuklia wa Iran Mohesn Fakhrizadeh kuuawa katika mazingira ya kutatanisha nje ya mji mkuu wa nchi hiyo Tehran Ijumaa iliyopita.

Iran inaamini kuwa Israel na kundi la Wairan walioiasi nchi na kukimbilia uhamishoni walitumia silaha inayodhibitiwa kwa remote kumuua mwanasayansi huyo.

Israel haijajibu madai hayo dhidi yake.

Fakhrizadeh alikuwa na mchango muhimu katika mpango wa kinyuklia wa Iran ambao serikali inasisitiza kuwa shughuli zake za kinyuklia ni kwa ajili ya amani na sio kutengeza silaha za kinyuklia zinazouweka ulimwengu katika hatari.

Rais wa Marekani Donald Trump chini ya utawala wake alirejesha vikwazo vikali vya kiuchumi dhidi ya Iran akikosoa makubaliano yaliyofikiwa kwa kuyataja yenye mapungufu makubwa na yanayoipa Iran nguvu za kutengeza silaha za kinyuklia.

Rais Mteule wa Marekani Joe Biden ameahidi kuirejesha nchi yake kwa makubaliano hayo yaliyofikiwa wakati wa utawala wa Rais Barack Obama.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *