img

Iran iko tayari kubadilishana wafungwa na nchi nyingine

December 3, 2020

Iran imesema iko tayari kuingia kwenye hatua ya kubadilishana wafungwa zaidi na nchi nyingine baada ya wiki iliyopita kumkabidhi kwao mfungwa Msomi Muingereza mwenye asili ya Australia na kupokea raia wake watatu waliokuwa wamefungwa katika jela za nje. 

Tangazo hilo amelitowa waziri wa mambo ya nje Mohammed Javad Zarif hii leo ambapo amezungumza mbele ya mkutano wa kidiplomasia wa Italia uliofanyika kwa njia ya video na kusema siku zote wako tayari kushiriki katika mpango huo na kwamba ni mpango wenye maslahi kwa kila mmoja. 

Kadhalika Zarif ameitolea mwito Marekani kuonesha nia njema kwa kurudi kwenye makubaliano ya kimataifa ya Nyuklia ya mwaka 2015 ambayo rais Donald Trump aliyapiga kumbo. Amesema ikiwa nchi hiyo itaheshimu ahadi zake za mwanzo, Tehran itatoa ushirikiano kikamilifu kwenye makubaliano hayo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *