img

Harmonize amuonyesha mtoto wake

December 3, 2020

Ni ‘updates’ za msanii Harmonize ambaye siku ya leo ameshea picha ya mtoto wake wa kwanza wa kike ambaye amemtambulisha kwa jina la Official Zulekha Kondegirl aliyempata mzazi mwenziye Official Nana Shanteel.

Kupitia Instagram Harmonize ameandika ujumbe mzito unaoeleza kuwa 

“Kweli humuweka yeyote huru haijalishi ni kiasi gani au muda gani ila naamini kusema hili litafanya moyo wangu uwe huru na nijione muungwana mbele ya Mungu na wewe unayesoma, pia muungwana zaidi mbele ya mtoto wa wangu kipenzi Zuu, nianze kusema samahani kwa kutojivunia wewe kwa mwaka mmoja na miezi 7” 

“Nisamehe pia kwa kutokuwa na ‘time’ hata ya kuja kukuangalia pale ulipokuwa unaumwa, kwa kuhofia kuvunja mahusiano ambayo nayaheshimu sana, tumepitia mengi na naamini kuchezea wanawake au kubadili sio sifa, hili suala limenitesa kwa muda rrefu, hadi ikafika pahala nikasema namuachia Mungu” 

“Nakuomba msamaha hadharini na nakuahidi kukupa moyo wangu wote, kwani hukuja kwenye hii dunia kwa bahati mbaya ni mpango wa Mungu nakupenda malkia wangu umenifanya nijione mtu mzima, nimejifunza na natarajia kujifunza mengi  kupitia wewe Official Zulekha Kondegirl, nilishasema ‘privately’ na nasema tena hadharani nisamehe mke wangu nina imani utalipoke kibinadaam” ameongeza 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *