img

Halima Mdee, Bulaya na Kishoa wabadili Wakili

December 3, 2020

Wabunge wa viti maalumu (Chadema), Halima Mdee, Ester Bulaya na Jesca Kishoa, wamemtambulisha wakili mpya atakayewatetea katika kesi yao ya mashtaka saba likiwemo la kufanya mkusanyiko na kutotii amri halali katika gereza la Segerea Jijini Dar es Salaam.

Wabunge hao ambao hivi karibuni walitangazwa kuvuliwa uanachama na Kamati Kuu ya Chadema leo Desemba 3, 2020 wamefika katika Mahakama ya Hakimu Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kesi ya kusomewa maelezo ya awali, wamewakilishwa na wakili Emmanuel Vkandis

Wabunge hao wanashtakiwa Mahakamani hapo na wenzao 24 ambao wote kwa pamoja hapo awali washtakiwa hao wote walikuwa wakitetewa na wakili Hekima Mwasipo.

Hata hivyo Mahakama imeshindwa kuwasomea washtakiwa hao kusomewa maelezo yao ya awali na badala yake imetoa hati ya kukamatwa kwa washitakiwa wawili, Edgar Adelini, Reginald Masawe, ambao hawajafika Mahakamani hapo leo bila taarifa yoyote. 

Mapema wakili wa serikali Ester Martin alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, kuwa kesi hiyo leo imeitwa kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali lakini washtakiwa wawili hawajafika hivyo wameomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea maelezo hayo na pia wameomba hati ya kukamatwa kwa washtakiwa hao.

Kati ya mashtaka hayo saba yanayowakabili, matatu ni ya kutoa lugha ya kuudhi yanayowakabili, Mdee, Bulaya na Jacob, moja ni kuharibu Mali, kufanya mkusanyiko usio kuwa wa halali, kutotii amri halali iliyowekwa na Jeshi la Magereza na shambulio.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *