img

George Lwandamina mrithi wa Cioaba Azam FC

December 3, 2020

George Lwandamina ambaye alikuwa kocha wa Yanga leo Desemba 2 ametua rasmi kwenye ardhi ya Bongo akitokea Zambia kwa ajili ya kuinoa Azam FC akichukua mikoba ya Aristica Cioaba.

Cioaba ambaye alikuwa ndani ya Azam FC kuanzia mwanzo wa msimu alifutwa kazi Novemba 26, siku moja baada ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga Uwanja wa Azam Complex. 

Kwa sasa timu ipo mkoani Mwanza ambapo Desemba 7 itakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Gwambina FC, Uwanja wa Gwambina Complex ikiwa chini ya kaimu kocha msaidizi, Vivier Bahati.

Akizungumza muda mfupi baada ya kutua Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Lwandamina amesema kuwa amekuja ndani ya Azam FC kufanya kazi hivyo mashabiki wampe sapoti.

“Nimefurahi kuja tena ndani ya Tanzania, nilikuwepo nikaondoka na sasa nimerudi tena, imani yangu ni kwamba tutakuwa pamoja katika kufikia mafanikio,” amesema.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *