img

DC, Naibu Spika wawapika madiwani Jiji la Mbeya

December 3, 2020

 Baada ya kula kiapo cha uadilifu, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson na mkuu wa Wilaya ya Mbeya, William Ntinika wamewakumbusha madiwani kuachana na tofauti  zao badala yake  wajielekeze kuwatumikia wananchi.

 Dk Tulia ambaye ni mbunge wa Mbeya Mjini amewataka madiwani hao kuitekeleza ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/25. Ametoa ushauri huo leo, Desemba 3 baada ya wawakilishi hao wa wananchi kuapa kuwatumikia wananchi.

“Hatutohitaji diwani anayefika kwenye vikao akiwa na mawazo yake binafsi…vikao vinavyofuata ni kuleta hoja za wananchi ili nami niweze kuziwasilisha katika vikao vya Bunge mjini Dodoma,” amesema.

Dk Tulia amesema kwa kiapo walichoapa, madiwani hao wanapaswa kutumia nafasi zao kuwa chachu za kuwasilisha mpango mkakati wa utekelezaji wa miradi kwa kushirikisha wananchi.

Mkuu wa wilaya hiyo, William Ntinika amewakumbusha madiwani hao kusimamia mapato ya halmashauri hususan miradi ya maendeleo.

“Serikali tunatambua fedha zilizopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya, hatuhitaji kusikia zinapungua kwa maslahi binafsi. Mkawe chachu ya kuongeza mapato,” amesema.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *