img

China yaongeza ushawishi kulilenga timu ya Biden

December 3, 2020

Dakika 6 zilizopita

A woman sets up Chinese and US flags in Beijing, 2014

Maelezo ya picha,

Hivi karibuni Marekani na China wamekuwa na mizozo ya kujirudia , kuhusu biashara na mlipuko wa virusi vya corona pamoja na Hong Kong

Mawakala wa China wameongeza juhudi zao kushawishi utawala unaokuja wa Rais mteule Joe Biden, afisa wa ujasusi wa Marekani amesema.

William Evanina, kutoka ofisi ya mkurugenzi wa upelelezi wa Marekani amesema Wachina walikuwa wananalenga pia watu walio karibu na timu ya Bwana Biden.

Bwana Evanina alisema hayo wakati wa kampeni ya ushawishi inayojulikana kama “on steroids”.

Tofauti na hayo, afisa wa idara ya haki alisema zaidi ya mawakili 1,000 wanaoshukiwa kuwa Wachina wamekimbia Marekani.Katika majadiliano, siku ya Jumatano taasisi ya Aspen, Bwana Evanina, Mkurugenzi wa Tawi la Upelelezi la Kitaifa, alisema Wachina walikuwa wakijaribu kuingilia kati juhudi za wamarekani kupata chanjo ya homa kali ya mapafu(corona) pamoja na uchaguzi wa hivi karibuni wa Marekani.

“Tumeona pia hali ya juu, ambayo ilipangwa na tulitabiri, kwamba China sasa itaongeza tena kampeni zao za ushawishi kwa utawala mpya wa [Biden].”Na ninaposema hivyo, ushawishi mbaya wa kigeni, ushawishi huo wa kidiplomasia , tunaanza kuona mchezo huo nchini kote sio watu tu wanaoanza katika utawala mpya, lakini wale walio karibu na watu hao. katika utawala mpya.

US President Donald Trump and Chinese President Xi Jinping

Maelezo ya picha,

Rais Donald Trump alimshutumu rais Xi Jinping wa China kueneza virusi vya corona

Kwa hivyo hilo ni eneo moja tutakuwa na hamu kubwa ya kuhakikisha kuwa utawala mpya unaelewa ushawishi huo, jinsi inavyoonekana, inavyopendeza, inahisije unapoiona. “Wote Bw Biden na Rais Donald Trump walipata mashtaka makali wakati wa kampeni ya hivi karibuni ya Ikulu ya kushawishiwa na Beijing.Bwana Trump alizingatia shughuli za kibiashara na mtoto wa mpinzani wake Hunter Biden nchini China, wakati mgombea wa Kidemokrasia aliangazia akaunti ya benki ya Bw Trump ya China.

Wakati wa mjadala huo wa jaribio la kufikiria Jumatano, John Demers, mkuu wa idara ya usalama idara ya usalama wa kitaifa, alisema mamia ya watafiti wa China walio na uhusiano na jeshi la nchi yao waligunduliwa na wachunguzi wa FBI wakati wa kiangazi.

Bwana Demers alisema uchunguzi huo ulianza wakati maafisa wa Marekani walipokamata watafiti watano au sita wa Wachina ambao walikuwa wameficha uhusiano wao na Jeshi la ukombozi wa watu (PLA)

Hao watano au sita waliokamatwa walikuwa ni ncha ya bonge la barafu na kiuweli ukubwa wa bonge hilo la barafu siwezi kuelezea jinsi walivyo ” alisema”.

Katika majadiliano alisema kwamba baada ya FBI kufanya mahojiano mengi na watu wengine, “zaidi ya watafiti 1000 wa kutoka China washirika wa PLA wameondoka nchini”.

Bwana Demers alisema “ni Wachina pekee wana rasilimali , uwezo na nia” ya kufanya ujasusi huo unaodaiwa kuwa wa kisiasa na kiuchumi na ” shughuli nyingine mbaya”.

Alisema katika majadiliano kuwa hawa watafiti ni nyongeza katika kundi la Wanafunzi wa Kichina 1000 na watafiti ambao viza zao zilifutwa na Marekani tangu Septemba.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *