img

China yaishutumu Marekani kuhusu sheria mpya ya VISA kwa Wachina

December 3, 2020

China imewashutumu wakosoaji wake katika serikali ya Marekani kwa kuongeza ukandamizaji wa kisiasa dhidi ya serikali yake. 

Tamko hilo la China linafuatia ripoti za kutangazwa sheria mpya za utolewaji Visa kwa wanachama wa chama cha kikomunisti cha China pamoja na watu wa familia zao. 

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Hua Chunying amesema nchi yake itawasilisha mtazamo wake nchini Marekani kufuatia ripoti hiyo iliyotangazwa Alhamisi katika gazeti la New York Times. 

Katika ripoti hiyo Marekani imeeleza kwamba Wachina ambao ni wanachama wa chama cha Kikonunisti na familia zao, Visa ya kuingia Marekani wanayoweza kupewa ni ya mwezi mmoja tu na ya kuingia mara moja. 

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, Hu ameeutaja mwelekeo huo wa Marekani kuwa ni hatua inayokwenda kinyume kabisa na Maslahi yake yenyewe na itaiharibia sifa nchi hiyo duniani.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *