img

Biden akutana na wafanyabiashara wadogo wadogo walioathiriwa kimapato kutokana na Corona

December 3, 2020

Rais mteule wa Marekani Joe Biden amefanya mkutano kwa njia ya video na wafanyabiashara wadogo wadogo na wafanyakazi ambao wameathiriwa pakubwa kiuchumi kutokana na janga la virusi vya Corona.

Biden amesimamia mkutano huo kutoka nyumbani kwake – Wilmington, Delaware, ambapo anafanyia shughuli zake za kujitayarisha kuingia madarakani baada ya kuapishwa Januari 20.

Vile vile, anaendele kupokea taarifa za kila siku kutoka kwa maafisa wa ujasusi wa Marekani kuhusu usalama nchini Marekani na sehemu nyingine zinazoangaziwa sana duniani.

Biden anakabiliwa na changamoto kubwa ya uchumi ambao umedorora kutokana na janga la virusi vya Corona atakapoingia madarakani hata wakati kuna matarajio ya kuanza kutolewa chanjo dhidi ya virusi hivyo baadaye mwezi huu.

Kulingana na chuo kikuu cha Johns Hopkins, maelfu ya watu wanaripotiwa kuambukizwa virusi vya Corona nchini Marekani kila siku, watu 272,000 wamefariki.

Marekani inaongoza kwa idadi ya vifo na maambukizi kutokana na Corona kote duniani.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *