img

Bangi sio tena dawa hatari yasema Umoja wa Mataifa

December 3, 2020

Umoja wa Mataifa imepiga kura kuondoa bangi katika orodha ya kundi la dawa hatari zaidi hatua ambayo inatambua mmea huo kwa manufaa yake kitiba.

Tume ya Umoja wa Mataifa ya kudhibiti dawa za kulevya, imeidhinisha pendekezo la Shirika la Afya Duniani- WHO, Jumatano la kuondoa bangi na utomvu wa bangi kutoka kwa kundi la dawa zenye kuhitaji kudhibitiwa ambapo imekuwa kwa kipindi kirefu.

Dawa katika kundi hili linalojulikana kama ‘Schedule IV’ huchukuliwa sio tu “za kulevya lakini pia zinazofanya mtu kuwa mtegemezi,” pia huchukuliwa kuwa “hatari na matumizi yake kimatibabu husemekana ni kwa kiwango kidogo sana.”

“Hizi ni habari njema kwa mamilioni ya watu wanaotumia bangi kama dawa na pia kuna akisi ukuaji wa soko la bidhaa hiyo kwa misingi ya kimatibabu,” kundi moja la utungaji wa sera za dawa limesema katika taarifa yake iliyotoa kwa wanahabari.

Kati ya nchi wanachana 53, ni 27 walipiga kura kuunga mkono huku 25 wakipinga kutambuliwa kwa bangi kama yenye manufaa huku Ukraine ikijuzuia kupiga kura.

Marekani na nchi za Ulaya ni miongoni mwa zile zilizopiga kura kuunga mkono, huku China, Misri, Nigeria, Pakistan na Urusi zikiwa miongoni mwa nchi zilizopinga utambuzi huo.

Hatua hiyo ya kihistoria inatarajiwa kufungua milango kwa mmea huo wa bangi kutambulika kwa munufaa yake kama dawa na tiba na pia itakuwa rahisi kwa nchi kufanya utafiti.

Bangi imekuwa katika orodha ya mimea inayodhibitiwa sana kwa miaka 59 na kuhamasisha watu ulimwenguni kutoitumia isipokuwa tu kwa matumizi ya tiba

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *