img

Bangi haipo tena katika orodha za dawa hatari, Umoja wa Mataifa

December 3, 2020

Waziri wa habari wa Somali Osman Abukar Dubbe ameshutumu Kenya kwa njama ya kupanga kuikosesha Somali amani wakati inajitayarisha katika uchaguzi wa urais, kituo cha televisheni kinachomilikiwa na serikali kimeripoti.

“Tunaheshimu Kenya, tunafurahia ujirani wetu na maslahi ya pande zote mbili. Upande wetu, kanuni na misingi yetu tunaidumisha. Hata hivyo, Kenya inaonekana kutojali hilo na badala yake inataka kutekeleza mambo yasiofaa na ni nchi ambayo dhamira yake ni kuchukua ardhi na sehemu ya majini ya Somali,” Bwana Dubbe amewaambia wanahabari katika matangazo ya moja kwa moja kupitia televisheni ya taifa kwa njia ya kurasa ya Facebook.

Waziri huyo ameishutumu Kenya kwa muingilio wa kisiasa na kuwa mwenyeji wa viongozi wa upinzani katika jiji la Nairobi.

Wanasiasa kutoka kusini mwa Somali eneo la Jubbaland, ni miongoni mwa wale ambao wamewahi kufanya mikutano mjini Nairobi huku majadiliano ya uchaguzi wa Somali mwaka 2020/2021 yakiendelea.

“Mogadishu haijawahi kuwa mwenyeji wa mwanasiasa yeyote wa upinzani kutoka Kenya, ambaye anataka kuharibu amani ya jirani zetu, lakini badale yake, Nairobi imekuwa ngombe ya mashambulizi yote dhidi ya Somalia. Pia imekuwa eneo ambalo makubaliano yote yaliyofikiwa ndani ya Somali yanakiuka.

Dubbe pia alisema kundi la kigaidi la al-Shabab liliteka maeneo kusini mwa Somalia baada ya wanajeshi wa ulinzi wa Kenya ambao ni sehemu ya wanajeshi wa Umoja wa Afrika Somalia (Amisom) kujiondoa kutoka kwa miji ya kimkakati eneo hilo.

Novemba 30, serikali ya Somali ilimuita nyumbani balozi wake nchini Kenya na pia ikamtaka balozi wa Kenya nchini humo “kuondoka kwa ajili ya majadiliano”.

Hata hivyo, Waziri wa mambo ya nje wa Kenya amekanusha taarifa hizo kuwa nchi hiyo inaingia masuala ya ndani na ya kisiasa ya Somalia.

Uhusiano kati ya Kenya na Somali umekuwa ukizorota katika miaka ya hivi karibuni hasa kwa mgogoro ya majini zaidi ya kilomita 150,000 za mraba katika Bahari Hindi eneo ambalo lina utajiri wa mafuta na gesi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *