img

Azaliwa baada ya mimba yake kutungwa miaka 27 iliyopita

December 3, 2020

Dakika 5 zilizopita

Molly Gibson

Maelezo ya picha,

Akiwa bado hajatimiza miezi miwili, Molly Gibson tayari ameweka rekodi

Wakati Molly Gibson alipozaliwa mwezi Oktoba mwaka huu, ilikuwa ni baada ya mimba yake kutungwa miaka 27 iliyopita .

Kiini tete chake (kuunganishwa kwa yai la mwanamke na mbegu za kiume katika maabara) kilikuwa kimewekwa kwenye friji mwezi Oktaba 1992, na kuishi humo hivyo hadi mwezi wa Aprili mwaka 2020, wakati Tina na Ben Gibson wakazi wa Tennessee walibokiasili.

Molly anaaminiwa kuweka rekodi mpya ya kiini tete kilichowahi kuishi kwa muda mrefu zaidi ndani ya friji ambacho kiliweza kuleta matokeo ya kuzaliwa kwa mtoto , akivunja rekodi ya dada yake mkubwa, Emma.

“Tunajihisi kana kwamba tuko juu ya mwezi ,” Alisema Bi Gibson . “Bado huwa ninapigwa na butwaa .”

“Ungeniuliza miaka mitano iliyopita kama sitakuwa na msichana mmoja bali wawili, ningesema we ni mwendawazimu ,” alisema.

Famili yake ilihangaika sana kuweza kupata mtoto kwa miaka karibu mitano kabla ya wazazi wa Bi Gibson kuona taarifa kuhusu uasili wa kiini tete katika kituo kimoja cha habari.

“Hiyo ndio sababu pekee inayotufanya tuwasimulie watu wengine kuhusu taarifa hii. Kama wazazi wangu wasingeona hili katika taarifa za habari basi tusingekuwa hapa.

Bi Gibson mwenye umri wa miaka 29, ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi na muma wake mwenye umri wa miaka 36-mchambuzi wa usalama wa Mtanda , waliwasiliana na kituo cha kitaifa cha viini tete -National Embryo Donation Center (NEDC), kituo cha Kikristo kinachotoa huduma bure katika mji wa Knoxville ambacho huhifadhi viini tete katika friji ambavyo wazazi waliopata watoto kwa usaidizi kimaabara(IVF) walioamua kutovitumia viini tete vyao vilivyosalia na badala yake kuamua kuvitoa kama msaada.

Familia kama ya Gibson inaweza baadae kuasili moja ya kiini tete kilichosalia na kumzaa mtoto ambaye unauhusiano wao wa jeni.Inakadiliwa kuwa kuna viini tete vya binadamu milioni moja vilivyohifadhiwa katika barafu nchini Marekani, kulingana na NEDC.

Mkurugenzi wa NEDC wa masuala ya masoko na maendeleo Mark Mellinger ,alisema kuwa uzoefu wa watu kutokuwa na uwezo wa kupata watoto ni jambo la kawaida katika familia ambazo zinataka misaada ya viini tete (Embyro).

“Ninaweza kusema labda 95% wame wamekabiliana na aina fulani ya kutokuwa na uwezo wa kupata mtoto “, alisema. “Tunahisi heshima na wenye bahari kufanya kazi hii” na kuwasaidia wanandoa hawa kukuza familia zao.

Baada ya kuasili kiini tete chao cha kwanza , Bi Gibson aliweza kujifungua mtoto wa kike Emma mwaka 2017, na kubadilisha maisha ya kukosa usingizi wa usiku kwa tkutamani mtoto na badala yake alianza kushindwa kusinzia kwa kumhudumia mtoto mchanga . “Ni aina bora ya mchoko ni aina nzuri sana ya mahangaiko ,” alisema.

Tina Gibson reads to her daughter, Emma

Kikianzishwa miaka 17, iliyopita kituo cha kuhfadhi viini tete vya binadamu cha NEDC kimeweza kimeweza kusaidia uasili wa viinitete 1,000 na kuzaliwa kwa watoto, na sasa kinahamisha viini tete 200 kila mwaka .

Sawa na mchakato wa kuasili, wanandoa wanaweza kuwamua kama wangependa uasili wa “siri ” wa kiini tete au wa “wazi” – kwa kuruhusu kuwa na mawasiliano ya aina fulani na familia iliyotoa kiini tete.

Mawasiliano haya huwa kuanzia barua pepe kadhaa za kila mwaka sawa na mahusiano ya mabinamu, alisema Bw Mellinger.

Mke na mume hupewa maelezo kati ya 200-300 ya mtoaji wa kiini tete, na kukamilishwa na historia ya maeneo walikoishi . Familia ya Gibson walitaka mtoto kwa muda mrefu, walikuwa na mambo mengi ya kuchagua.

“Hatukujali huyu mtoto atafananaje, wala anatoka wapi ,”Anasema Bi Gibson . Aliomba ushauri kutoka katika kituo cha NEDC ambako mfanyakazi wake alimwambia achague kitu cha “kawaida” na aanzie hapo, asifikirie sana.

“Mimi na mume wangu ni watu wadogo, na kwahiyo tulitafuta kitu kinachofanana na sisi ,” alisema.

Baada ya miaka kadhaa ya kutafuta nilibaini kuwa dada yangu mlango wa pili.
Maelezo ya picha,

Baada ya miaka kadhaa ya kutafuta nilibaini kuwa dada yangu mlango wa pili.

Watoto wa Gibson, Molly na Emma, ni ndugu wa kimaumbile. Viini tete vyao vilitolewa na kuwekwa katika friji kwa pamoja mwaka 1992, wakati Tina Gibson alipokuwa na umri wa mwaka mmja.

Kulingana na NEDC, kiini tete cha Emma cha umri wa miaka 24-kilikuwa ndio chenye umri wa miaka mingi katika historia kuwahi kuzaliwa, hadi Molly alipozaliwa mwaka huu.

Emma anampenda dada yake mdogo, anasema Bi Gibso.

” Huwa anamtambulisha kwa kila mtu anayemuona kama ‘dada yangu mdogo Molly.’”

Na Bi Gibson amefurahi kuona vitu vinavyofanana kati ya madada hao wili , ikiwa ni pamoja na kunyanzi dogo kati kati ya macho yao wanapokasirika

Kwamujibu wa kituo cha NEDC ,kiini tete kinaweza kutunzwa kwa muda mrefu.

Hatahivyo kutokana na enzi hii ya teknolojia – mtoto wa kwanza aliweza kuzaliwa kutokana na kiini tete kilichowekwa kwenye friji baada ya IVF alizaliwa nchini Australia mwaka 1984.

“Inawezekana kwamba kutakuwa na siku moja ambapo mtoto ataweza kuzaliwa kutokana na kiini tete kilichotunzwa kwenye barafu kwa miaka 30.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *