img

Waziri Mkuu wa Thailand afutiwa mashitaka ya ukiukaji wa maadili

December 2, 2020

Mahakama ya katiba nchini Thailand imemfutia mashitaka Waziri Mkuu Prayuth Chan-ocha ya kukiuka vifungu vya maadili katika katiba ya nchi hiyo, na hivyo kumruhusu kubaki katika wadhifa wake. 

Mahakama hiyo ambayo ndiyo ya juu kabisa imefanya uamuzi huo kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa na chama cha Pheu Thai, ambacho ndicho kikubwa kabisa cha upinzani bungeni, kuwa Prayuth alivunja sheria kwa kuendelea kuishi katika makazi yake ya kijeshi baada ya kustaafu kama kamanda wa jeshi mnamo Septemba 2014. 

Uamuzi huo unakuja wakati Waziri Mkuu huyo akikabiliwa na maandamano yasiyo na kikomo ya vuguvugu la kuunga mkono demokrasia linaloongozwa na wanafunzi likimtaka yeye na serikali yake kujiuzulu, likihoji kuwa waliingia madarakani kinyume cha sheria. 

Mahakama hiyo ya katiba, kama tu lilivyo jeshi, inachukuliwa kama nguzo ya utawala wa kifalme wa nchi hiyo na ngome ya mwisho dhidi ya vitisho vinavyotolewa kwa utawala huo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *