img

Waziri Harouni awataka watendaji wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kutimiza wajibu wake

December 2, 2020

 

Waziri wan chi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumushi na Utawala Bora Mhe Haroun Ali Suleiman amewahimiza watendaji wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake wa majukumu yake ya kiutendaji 

Haroun ameyasema hayo wakati alipokutana na Mwanasheria  Mkuu pamoja na  watendaji wa Ofisi hio pamoja na wafanyakazi  ikiwa ni utaratibu wa kukutana na viongozi wa Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora mara baada ya kuapishwa 

Mhe Haroun amesema jukumu kubwa liliopo ni kuhakikisha kila mtendaji anawajibu wa kusimamia majukumu yake na kuweka mbele maslahi ya taifa ikiwemo  kuwa mzalendo wa kweli , kuwa muadilifu, kujenga uaminifu na kusimamia vyema majukumu ya Serikali  wakiamini  Zanzibar itajengwa na wazanzibari wenyewe 

‘Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ni Taasisi kubwa hivyo watendaji  hakikisheni  wafanyakazi mnawasomesha , zinapokuja fursa za ndani na nje ya nchi mnawapa wafanyakazi ili waingie katika ushindani  wa kitaalamu wa fani mnayoifanyia kazi  masuala ya Sheria na Katiba ndio yanayoipa sura nchi na ndimo kunakonekana utawala bora  kubwa Zaidi ya yote hakikisheni  mnashinda kesi za Serikali  hii ndio faida ya kuwa na wataalamu wazalendo’alisisitiza mwalimu Haruon

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt Mwinyi Talib amemuhakikishia waziri pamoja na wafanyakazi kuwa ataendelea kusimamia vyema majukumu aliyopangiwa ikiwemo maslahi yao na kuondosha manunguniko ili ufanisi uwe bora zaidi 

Aidha ameahidi kuandaa mpango kazi wa miaka mitano utakaoonesha utekelezaji,uchambuzi wa  bajeti na matumizi yake, majukumu ya watendaji na wafanyakazi, vitendea kazi na vyanzo vya mapato ili kukamilisha ujenzi wa jengo la Ofisi hio kwa Unguja na Pemba katika kiwanja kipya kinachotegemwa kujengwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kilichopo Tibirinzi  Chake Chake

‘sambamba na hili Ofisi  ya  Mwanasheria Mkuu imeanza kutayarisha mpango mkakati wa miaka kumi baada ya Mpango Mkakati wake uliopo kumaliza muda ambapo rasimu ya awali imeshawasilishwa kwa mshauri elekezi wa Afisi yetu’ alisema Dkt Mwinyi 

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji Mkurugenzi Mipango, Uendeshaji na Rasilimali watu Bi Hamisa Mmanga amesema kwa kipindi cha Julai hadi Septemba  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu imeandaa  jumla ya kanuni 13 zinazotokana na sheria tofauti ili ziweze kutekelezeka, kuchapisha nakla 500 za Katiba ya Zanzibar 1984 pamoja na marekebisho yake hadi 2016 na kugaiwa kwa taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo Baraza la Wawakilishi, Baraza la Mapinduzi, Mahakama na taasisi nyengine

Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar 1964 Mwanasheria Mkuu ndio Mshauri Mkuu wa Serikali kwa mambo yote ya Kisheria 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *