img

Wanafunzi wa shule za msingi Rahaleo na Shangani wapewa elimu ya matendo ya ukatili wa kijinsia.

December 2, 2020

Na Faruku Ngonyani,Mtwara

Kuelekea kilele cha siku ya kupinga matendo ya ukatili wa kijinsia tarehe 10 Diemba 2020kituo cha msada wa wa kisheria Mkaoni Mtwara (Paraligo) kwa kushirikiana na Taasisi ya PWY wametoa elimu kwa wanafunzi wa Shule za Msingi Rahaheo na Shangani zilizopo Manispaa Mtwara Mikindani ili waweze kutambua haki zao.

Makamu Mwenyekiti kutoka kituo cha msaada wa kisheria Tunda Stambuli amesema kuwa ikiwa tukiwa kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga matendo ya ukatili wa kijinsi wametembelea shule hizo ili kuzungumza na wanafunzi hao ili waweze kutambua matendo wanayotendewa pindi wawapo nyumbani .

Aidha Tunda amevitaja baadhi ya vitendo hivyo vinavyowakabili baadhi ya wanafunzi Mkoani Mtwara  ikiwa pamoja na kupigwa ,ubakiji, pamoja na kuolewa wakiwa na  umri mdogo.

Lakini pia Tunda amechukua fursa hiyo kwa kutoa wito ka jamii kuwa na kawaida ya kutoa taarifa kwenye vyombo vinavyohusika pindi wanapokuwa wanaona matendo ya ukatali wa kijinsi katika maeneo yao.

Kwa upande wa wanafunzi waa Shule hizo wameikea elimu hiyo huku wakiahidi kuripoti matendo yatakayoshiria vunjifu wa ukatili kijinsia .

Ikumbukwe maadhimisho ya siku ya kupingamatendo ya ukatili wa kijinsia itaadhimishwa tarehe 10 Disemba 2020. 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *