img

Waislamu wanakabiliwa na shinikizo la kuukubali utamaduni wa Kifaransa

December 2, 2020

Dakika 5 zilizopita

Sallah a babban masallacin birnin Paris, 30 ga watan Octoba 2020

Maelezo ya picha,

Sala katika msikiti mkubwa wa Paris

Wiki hii Baraza la Waislamu nchini Ufaransa (CFCM) liko tayari kukutana na rais Emmanuel Macron, kuidhinisha nyaraka mpya za ” Sheria ya utamaduni ya Ufaransa ” ambayo maimamu wanatakiwa kusaini.

Inaripotiwa kuwa baraza hilo (CFCM), linalojumuisha makundi mbalimbali ya Waislamu nchini humo linatakiwa kujumuisha katika nyaraka hizo sheria ya utamaduni wa Kifaransa , ya Jamuhuri ya Ufaransa, inayojumuisha kukataa dini ya Kiislamu kama chama cha kisiasa na kuzuwia ushawishi wa kigeni.

“Sote hatukubali kuhusu kilichomo ndani ya sheria ya Ufaransa ,” amesema Chems-Eddine Hafiz, makamu rais wa CFCM ambaye pia ni mkuu wa msikiti mkubwa wa Paris- Paris Grand Mosque.

Hatahivyo, anasema kuwa, “tuko katikati ya mabadiliko ya historia ya Uislamu nchini Ufaransa na sisi kama Waisamu tunakabiliwa na wajibu .” Miaka minane iliyopita, alisema, mawazo yake yalikuwa tofauti.

Mwanamgambo wa kiislamu Mohamed Merah hivi karibuni alifanya shambulio katika mji wa Toulouse.

.”Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy alinifanya niamke kutoka kitandani karibu saa kumi na moja alfajiri kujadili suala hili. Nilimwambia : ‘Jina lake huenda likawa ni Mohammed, lakini pia ni mhalifu! Sikutaka kukanganya uhalifu na dini. Lakini leo, ninakanganya. Kasisi wa kifaransa anapaswa kushughulikia suala hili. “

Mpango ulikuwa ni kwa kikundi hicho cha viongozi wa Kiislamu kutengeneza usajili wa viongozi wa dini nchini Ufaransa ,ambapo kila mmoja wao atasaini sheria hiyo, kabla ya kuhojiwa.

Mwezi Oktoba, Rais Emmanuel Macron alizungumza dhidi ya “kuwapa shinikizo ” viongozi wa Kiisalmu.

Lakini pia ni vigumu kwa nchi ya yenye uongozi wa Kisha ambao wanataka kutofautisha dini na serikali.

Bw Macron anajaribu kuzuwia siasa za kiislamu, bila kulaumiwa kwa kuingilia masuala ya kidini au ubaguzi dhidi ya dini nyingine.

Kuyaleta pamoja makundi ya Kiislamu katika jamii ya Ufaransa limekuwa ni jambo muhimu katika miaka ya hivi karibuni .

Zanga-zanga ka dokar Faransa kan ska hijabi, Avignon, 3 ga watan Satumba 2016

Ufaransa inakadiriwa kuwa na waislamu milioni tano-ikiwa ni nchi yenye idadi kubwa ya Waislamu walio wachache barani Ulaya.

Olivier Roy, mtaalamu wa masuala ya Kiislamu nchini Ufaransa, anasema sheria inasababisha matatizo mawili.

Moja ni ubaguzi kwasababu sheria hii inawahusu wahubiri wa dini ya Kiislamu pekee, na lingine ni haki ya kuwa muumini wa dini.

“Unatakiwa kuheshimu sheria hizi za kitaifa ,” anasema, “lakini haupaswi kuwatenga wajumbe wa makundi ya wapenzi wa jinsia moja na waliobadili jinsia zao- LGBT, kwa mfano, Kanisa Katoliki halijaidhinisha ndoa ya wapenzi wa jinsia moja . ”

Mwanamitindo wa urembo nchini Ufaransa, Iman Mestaoui amekuwa kipokea jumbe zenye maneno makali kutokana na kile alichokiita “wanaomchukia ” – akimaanisha Waislamu wenye itikadi kali ambao wanasema mitindo yake ya mavazi mara nyingi haimstili mwanamke kwa kufunika kichwa chake vyema.

Hatahivyo, amesema, suala la kuwaamrisha viongozi wa dini kusaini “sheria ya Ufaransa” ni tatizo, ikizingatiwa kuwa Waislamu hawaangaliwi kama raia kamili wa Ufaransa.

“Ni kutuweka katika hali ambapo ni lazima uwaoneshe watu kwamba unakubali utamaduni wa Kifaransa na maadili yake, wakati unahisi kuwa ni Mfaransa, lakini pia haujihisi kuwa si Mfaransa mwilini mwako .”alifafanua.

Limami Hassen Chalghoumi

Maelezo ya picha,

Mchungaji Chalghoumi akiongoza maombolezo ya mwalimu Mfaransa aliyekatwa kichwa Samuel Paty.

“Tunahisi kana kwamba kila kitu tunachokifanya -iwe kodi, miradi ya ‘maendeleo’ – intatosha. Lazima uoneshe kwamba wewe ni raia wa Ufaransa; lazima ule nguruwe;unywe pombe;usivae hijab; uvae “Sketi fupi?. Hiyo sio sahihi .”

‘Itikadi kali na mabomu’

Lakini Hassen Chalghoumi, imam wa msikiti wa Drancy uliopo viungani mwa mji mkuu Paris, alisema baada ya miaka ya ugaidi, serikali ililazimishwa kuchukua hatua.

Bw Chalghoumi kwa sasa amejificha, baada ya kupokea vitisho dhidi yake kuhusiana na mawazo yake ya kufanyika kwa mageuzi.

“Lazima tushughulikie suala hili kikamilifu na kuonesha kwamba sote tumeungana, kwamba tunaheshimu sheria ,” aliiambia BBC. “Haya ni matokeo ya itikadi kali .”

“Sio uchokozi, ni haki ninayosema ,” alisema.

Nje ya msikiti mkubwa wa Paris – Paris Grand Mosque, Charki Dennai alipokuwa anafika msikitini kwa ajili ya ibada ya siku alisema:

“Hawa vijana wenye itikadi kali ni kama mabomu,” alisema huku akiwa amebeba mkeka wa kuswalia na Koran. Hiki ndicho ninachokifanya. Lakini kuna maswali kuhusu athari walizonazo maima kwa Waislamu vijana, hususan inapokuja katika ghasia za itikadi kali.

“Haitawezekana,” alisema Olivier Roy, “kwasababu magaidi hawakutoka katika msikiti wa Salafi.Ukiangalia utambulisho wa magaidi, hakuna hata mmoja aliyetoka anakofundisha Salafi ”

Mawazo ya Kisalafi ni ya kundi la itikadi kali lenye uhusiano na siasa ya dini ya Kiislamu.

Anti-Islamophobia rally in Toulouse, 27 Oct 19

Utatuzi wa tatizo la kupuuzwa kwa vijana

Sheria hiyo ni sehemu ya sera kubwa za serikali za kukabiliana na tatizo la ushawishi wa kigeni, kuzuwia ghasia na vitisho kutoka kwa watu wenye itikadi kali, na pia kuwavutia vijana wanaohisi kuwa wamepuuzwa nchini.

Bw Macron anaangalia uwezekano wa kuongezwa kwa mafunzo ya lugha ya kiarabu katika shule nchini Ufaransa na kuendeleza zaidi meneo yaliyoachwa nyuma kimaendeleo, na amekwisha tangaza wazi kwamba atakabiliana na wenye itikadi kali wanaoikataa sheria ya Ufaransa na utamaduni wan chi hiyo, lakini sio Waislamu wote.

Hakim El-Karoui ni mtaalamu kuhusu makundi ya Kiislamu ya Ufaransa katika kituo cha Montaigne ambacho mara kwa mara huchangia katika fikra za serikali.

Lakini anasema Waislamu wenyewe wanapaswa kuhusika katika shughuli za serikali, “kwasababu wanaweza kuchangia kutoa taarifa na uelewa kuhusu Uislamu katika mitandao ya kijamii -serikali imeshindwa kufanya hivyo .”

Na bila sahihi za “Waislamu wa vijijini “, Olivier Roy anasema, itakua vigumu kwa sheria mpya kutekelezwa.

“Serikali itafanya nini? “Tubadili katiba au tuvumilie mfumo wa ‘uhuru wa dini’ au serikali haitaweza kuwachaguliwa Waislamu kiongozi wao wa kidini.” Alisema.

Mwanamitindo ya urembo Iman Mestaoui aliiambia BBC mjini Paris kwamba familia yake yote ilimpigia kura Rais Macron katika uchaguzi wa mwaka 2017.

Lakini tangu wakati huo anasema, amegundua ”mabadiliko makubwa” katika uhuru wa usalama na masuala ya uhamiaji.

“Nilikuwa mfuasi wa Macron,” alisema .”Yalikuwa ni matumaini yetu katika jamii, lakini sasa ninahisi tumetengwa .

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *