img

Wabunge wa Israel wapitisha pendekezo la kulivunja bunge

December 2, 2020

Wabunge wa Israel wakiungwa mkono na mshirika mkuu wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu leo wamepitisha pendekezo la awali la kulivunja bunge katika hatua moja kubwa kuelekea kuitumbukiza nchi hiyo katika uchaguzi wake wa nne wa kitaifa chini ya miaka miwili. 

Kura hiyo ya bunge imekuja miezi saba tu baada ya muungano huo kuchukua uongozi katika tamko la umoja wa kitaifa la kupambana na janga la corona. Lakini tangu wakati huo, muungano kati ya chama cha Netanyahu cha Likud na cha Buluu na Nyeupe chake Waziri wa Ulinzi Benny Gantz umekumbwa na malumbano ya ndani yasiyokuwa na kikomo. 

Kura ya leo imetoa tu idhini ya awali ya kuumaliza muungano huo na kulazimisha uchaguzi mpya mapema mwakani. Mswada huo sasa unafikishwa mbele ya kamati kabla ya kurejeshwa bungeni ili kuidhinishwa kwa mara ya mwisho. Gantz na Netanyahu wanatarajiwa kuendelea na mazungumzo katika juhudi za mwisho za kuuokoa muungano huo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *