img

Virusi vya Corona: Uingereza kuanza matumizi ya chanjo ya corona

December 2, 2020

Dakika 6 zilizopita

chanjo

Uingereza limekuwa taifa la kwanza duniani kudhibitisha matumizi ya chanjo ya Pfizer/BioNTech dhidi ya virusi vya corona.

Mamlaka ya udhibiti nchini a Uingereza- MHRA, imesema chanjo hiyo inayotoa ulinzi wa asilimia 95% dhidi ya kuugua Covid-19, hivyo ni salama kuanza kutumika.

Chanjo hiyo itaanza kutumika siku chache zijazo na makundi ya watu walio katika hatari zaidi ya maambukizi watapewa kipaumbele.

Uingereza imeagiza dozi milioni 40 ambazo zitawatosheleza watu milioni 20, kwa kila mmoja kupata chanjo mara mbili.

Dozi zipatazo milioni 10, zitapatikana hivi karibuni .

Chanjo hii imedhitishwa haraka zaidi kwa matumizi kuliko chanjo nyingine yeyote, imechukua miezi 10 tu wakati kwa kawaida chanjo kudhibitishwa huwa inachukua miongo kadhaa.

Licha ya kwamba chanjo itaanza kutumika, watu watalazimika bado kufuata masharti ya kujikinga dhidi ya virusi vya corona, wataalamu wamesema.

Hii ni pamoja na kukaa kwa umbali , kuvaa barakoa na kufanya vipimo .

chanjo

Chanjo hii ni ipi ?

Ni aina mpya inayoitwa mRNA inayotumia alama za chembechembe za jeni ya urithi kutoka kwa virusi kuufundisha mwili jinsi ya kupamabana na Covid-19 na kujenga kinga ya mwili.

Chanjo ya mRNA haijawahi kuidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu awali, japo watu wamekuwa wakiipokea katika majaribio ya kimatibabu katika kliniki. Chanjo hii ni lazima itunzwe katika mazingira ya takriban nyuzijoto 70 na itakuwa ikisafirishwa katika maboksi maalum, yaliyowekwa katika barafu kavu.

Pale imapofikishwa katika eneo husika, inaweza kutunzwa hadi kwa muda wa siku tano ndani ya friji.

Ni nani atakayepewa chanjo hii na ni lini?

Wataalamu wameandaa orodha ya awali, wakiwalenga watu wanaokabiliwa na hatari zaidi iwapo watapatwa na corona.

Wa kwanza kabisa katika orodha hiyo ni watu wanaohishi katika nyumba wanaotegemea uangalizi na wahudumu wao, wakifuatiwa na watu wenye umri wa zaidi ya miaka 80 na wahudumu wengine ya kijamii na kiafya.

Watapokea shehena ya kwanza ya chanjo-baadhi yao wakizipata wiki ijayo.

Uchanjwaji wa watu wengi wenye umri wa zaidi ya miaka 50 , utafuatia pamoja na vijana wenye matatizo ya kudumu ya afya.

Shehena zaidi za chanjo zinaweza kuwepo mwaka 2021.

Chanjo hii hutolewa kwa sindano mbili kati ya siku 21 tofauti , huku dozi ya pili ikiwa ni ya kuimarisha chanjo ya awali.

Vipi kuhusu chanjo za Covid?

Kuna baadhi ya chanjo nyingine zinazotumainiwa kwamba zinaweza kuidhinishwa hivi karibuni.

Kuanzia Moderna inayotumia jina sawa na mRNA huku chanjo ya Pfizer pia ikitoa kinga sawa.

Uingereza imeagiza mapema chanjo milioni 7 ambazo zinaweza kuwa tayari kuanzia mwezi Aprili mwaka ujao .

Uingereza iliagiza dozi milioni 100 za aina tofauti za chanjo ya Covid kutoka Chuo kikuu cha Oxford na AstraZeneca.

Chanjo hiyo hutumia kirusi kisicho na madhara, kilichobadilishwa kufanana zaidi na virusi vinavyosababisha Covid-19.

Urusi imekuwa ikitumia chanjo nyingine, inayoitwa Sputnik, na jeshi la China limeidhinisha chanjo nyingine iliyotengenezwa na CanSino Biologics.

Zote zinafanya kazi sawa na chanjo ya Oxford .

Kampuni hii ya Pfizer/BioNtech ni ipi?

chanjo

Pfizer/BioNtech ni kampuni ya kwanza ya dawa kutoa maelezo kuhusu awamu ya mwisho ya kufanyia majaribio chanjo yake.

Matokeo yake inaashiria kuwa chanjo hiyo inaweza kumkinga mtu kutokana na Covid- 19 kwanza asilimia 90.

Karibu watu 43,000 wamepewa chanjo hiyo na hakuna visa vya hofu ya usalama wake vilivyoripotiwa.

Moderna ilifanyia majaribio ya chanjo yake kwa watu 30,000 nchini Marekani, ambapo nusu ya watu hao walidungwa sindano ya majaribio.

Inasema chanjo yake inatoa kinga ya asilimia 94.5 baada ya kutumiwa na watu watano wa kwanza kati 95 waliokua wameonesha dalili ya maambukizi ya Covid kupokea chanjo hiyo.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *