img

Ukiukaji wa sheria kwenye uchaguzi wa Bosnia

December 2, 2020

Polisi wameendesha operesheni katika miji ya Srebrenica na Tuzla nchini Bosnia Herzegovina, kutokana na ukiukaji wa sheria ulioripotiwa kuwepo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wa tarehe 15 Novemba.

Katika taarifa zilizotolewa na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Bosnia  Herzegovina,  iliarifiwa kuwa operesheni ilianzishwa baada ya kuripotiwa madai ya ukiukaji wa haki ya upigaji kura na utumiaji wa data binafsi bila kuidhinishwa.

Taarifa zaidi zimefahamisha kuwa operesheni iliendeshwa baada ya raia waliopiga kura nje ya nchi kutoa malalamiko yao, ingawa hakukutolewa maelezo ya kina kwa sababu za usalama wa suala hilo.

Tume  Kuu  ya Uchaguzi (CIK) ilitoa tangazo wiki zilizopita kwamba kura zote za Srebrenica, isipokuwa kura kutoka  nje ya nchi, zimehesabiwa na  Mladen Grujicic ambaye ni mgombea wa vyama vya vya Serbia anaongoza katika nafasi ya meya .

Wakati ajenda kuu huko Srebrenica kabla na baada ya uchaguzi ikiwa inahusu madai ya makosa yaliyofanywa na wananchi wa Serbia, ilidaiwa kuwa magari kadhaa yaliyokuwa na leseni za Serbia yalitumika kubeba wapiga kura kwenda Srebrenica siku ya uchaguzi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *