img

Uingereza kuanza matumizi ya chanjo ya corona

December 2, 2020

Uingereza limekuwa taifa la kwanza duniani kudhibitisha matumizi ya chanjo ya Pfizer/BioNTech dhidi ya virusi vya corona.

Mamlaka ya udhibiti nchini a Uingereza- MHRA, imesema chanjo hiyo inayotoa ulinzi wa asilimia 95% dhidi ya kuugua Covid-19, hivyo ni salama kuanza kutumika.

Chanjo hiyo itaanza kutumika siku chache zijazo na makundi ya watu walio katika hatari zaidi ya maambukizi watapewa kipaumbele.

Uingereza imeagiza dozi milioni 40 ambazo zitawatosheleza watu milioni 20, kwa kila mmoja kupata chanjo mara mbili.

Dozi zipatazo milioni 10, zitapatikana hivi karibuni .

Chanjo hii imedhitishwa haraka zaidi kwa matumizi kuliko chanjo nyingine yeyote, imechukua miezi 10 tu wakati kwa kawaida chanjo kudhibitishwa huwa inachukua miongo kadhaa.

Licha ya kwamba chanjo itaanza kutumika, watu watalazimika bado kufuata masharti ya kujikinga dhidi ya virusi vya corona, wataalamu wamesema.

Hii ni pamoja na kukaa kwa umbali , kuvaa barakoa na kufanya vipimo .

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *