img

TMA yataja mikoa saba kukumbwa na mvua kubwa kuanzia kesho

December 2, 2020

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa angalizo la uwezekano wa kunyesha mvua kubwa katika mikoa mitano ukiwamo wa Dodoma kuanzia kesho.

Angalizo hilo limetolewa leo Jumatano, Desemba 2, 2020 na mamlaka hiyo huku ikibainisha mikoa  mingine ni Njombe, Rukwa, Songwe, Singida, Mbeya na Iringa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, athari zinazoweza kujitokeza  ni pamoja na makazi kuzungukwa na maji na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *