img

Tetesi za soka kimataifa

December 2, 2020

 Manchester United, na Chelsea zinamfuatilia kwa karibu mlinzi wa Brighton Muingereza Ben White, 23 mwenye thamani ya juu. (Sky Sports)

Barcelona wanafuatilia kwa karibu upatikanaji wa kiungo wa kati -nyuma wa Arsenal Shkodran Mustafi, 28, na mlinzi wa Chelsea Antonio Rudiger, 27, huku wachezaji hao wa kimataifa wa Ujerumani wakiwa hawatakiwi na klabu zao. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Arsenal na Tottenham ni miongoni mwa klabu kadhaa zenye nia ya kumsaini kiungo wa kati wa Red Bull Salzburg Dominik Szoboszlai, 20, huku RB Leipzig, AC Milan na Atletico Madrid pia wakimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Hungary. (Eurosport)

Manchester United, Manchester City na Chelsea wanashindana kumsaini kiungo wa kati wa Borussia Monchengladbach na Uswiss Denis Zakaria, 24, mwezi Januari . (Star)

Tottenham bado wanamtaka mlinzi wa Inter Milan na Slovakia -Milan Skriniar, 25, licha ya mazungumzo kati ya klabu hizo kuvunjika msimu uliopita . (Football Insider)

Mlindalango wa Ajax na Cameroon Andre Onana, 24, anaweza bado kufanikiwa kuhamia katika klabu ya Primia Ligi msimu ujao baada ya Tottenham na Chelsea kuacha nia yao. (Mail)

Arsenal bado hawajaweka dau la kiungo wa kati wa Norwich Emi Buendia, 23, huku Muargentina huyo akiwa miongoni mwa wachezaji wanaoweza kuchaguliwa kusaini mkataba na the Gunners. (Football London)

Kiungo wa kati wa Arsenal Patrick Vieira, ambaye kwa sasa ni meneja wa klabu ya Nice, anataka kumleta katika klabu hiyo mchezaji wa Arsenal na Ufaransa-mlinzi William Saliba, 19. (Metro)

Juventus wanajiandaa kuongeza mara dufu dau lao kwa ajili ya kiungo wa kati -nyuma wa Chelsea Muitalia Emerson Palmeri, 26, na mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 34. (Il Bianco Nero – in Italian)

Barcelona wamechagua mlinzi wa Atletico Madrid na Brazil Felipe Augusto, 31, kama mchezaji wao kmbadala wa kuchukua nafasi ya Gerard Pique, 33, mwenye majeraha huku msimu wa Uhispania ukiwa umemalizika. (AS – in Spanish)

Mlinzi wa Ufaransa Jean-Clair Todibo, 20, yuko tayari kurejea katika Barcelona baada ya kushindwa kucheza hata dakika moja wakati wa mkataba wake wa mkopo katika Benfica. (Abola – in Portuguese)

Mchezaji wa safu ya kati wa Barcelona Riqui Puig, 21, ataruhusiwa kuondoka kwa mkataba wakati wa dirisha la uhamisho la wachezaji la mwezi Januari na mchezaji huyo wa timu ya Uhispani ya vijana walio chini ya umri wa miaka 21 amepewa fursa ya kuinga na Leeds United, RB Leipzig na Monaco. (Eurosport)

Rangers wanaonekana wako tayari kumkosa mchezaji asiye na wakala Muingereza Jack Wilshere, 28, huku wakitaka kiungo huyo wa kati arejee Arsenal. (Sun)

Arsenal wanaweza kutumia pauni milioni 32 iwapo wanataka kuendelea kuwa na wachezaji watano ambao mkataba wao unakamilika msimu ujao ili kuimarisha kikosi hicho katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari . (Football London)

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *