img

RC Tabora awataka viongozi kurudisha maji soko kuu

December 2, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dkt. Philemon Sengati ametoa wiki mbili kwa uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kuhakikisha wamerudisha maji katika Soko Kuu.

Dkt. Philemon Sengati alitoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kukagua masoko mkoani humo kwa ajili ya kujionea matatizo mbalimbali wanayokabiliana nayo wafanyabiashara. Ambapo aliwakuta wafanyabiashara wa soko hilo wakiendesha shughuli zao huku maji yakiwa yamekatwa.

 “Nataka hapa watu wapate maji ya uhakika ndani ya wiki mbili …angalie katika ‘strategic area’ muweke maeneo ya watu kupata maji ambayo yatawasaidia kufanya biashara zake bila matatizo” alisema RC Sengati

Aidha Dkt. Sengati alisema utatuzi wa tatizo la maji katika soko hilo na mengine lazima ufanyike haraka ili kulinda afya za wafanyabiashara hao huku akiuagiza uongozi wa  Manispaa ya Tabora kukutana na viongozi wa masoko ili kuweka mpango endelevu wa kuhakikisha maji hayakatwi na Mamlaka ya Maji kwa sababu ya watumiaji kushindwa kulipia bili.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *