img

Rc Byakwa; wananchi wa Mtwara mjitokeze tuichangie Ndanda ili tuinusuru

December 2, 2020

Na Faruku Ngonyani,Mtwara

Wadau wa michezo na wananchi Mkoani Mtwara wametakiwa kuichangia timu ya Ndanda inayoshriki Ligi daraja la kwanza hapa nchini ili kuinusuru kutokana na hali ya uchumi walionayo.

Wito huo pia umetolewa na mlezi wa timu hiyo ambaye pia Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa alipokuwa anazungumz na waandishi wa habari hii leo ofisini kwako.

Mlezi huyo amesema kuwa kwa sasa timu hiyo haina matokeo mazuri uwanjani inasabababishwa na club haina uwezo wa kuwalipa mishahara wachezaji wake, ubora wa wachezaji,jambo la tatu linatokana na miongozo ya shirikisho la mpira pamoja kutokuwa na mdhamini wa ligi daraja la kwanza hapa nchini.

Mlezi huyo ametoa wito kwa wanachi  wote Mkoani Mtwara kujitokeza kwa kuichangia timu ya NDANDA ili waweze kuinusuru na hali ya kiuchumi.

Mkuu huyo wa Mkoa ameongeza kuwa kwa yeyote mwenye nia njema ya kuichangia timu ya NDANDA aweke mchange wake kwa akaunti na ya CRDB 0150328948001 NDANADA SPORTS CLUB au kupitia Mpesa no 0757858417.

“Mimi Byakanwa mlezi wa timu ya Ndanda nawatangazia kuwa hali ya Ndanda kifedha ni dhoofu bini hali,mimi Mkuu wa Mkoa nimefanya kila hatua nimejitahidi na kamati yangu niliyounda  Naomba nitoe wito kwa wadau na wananchi wote wa Mtwara tujitokeze kuichangia Ndanda’’Byakanwa.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *