img

Rais wa Iran apinga mswada wa kuimarisha shughuli za nyuklia

December 2, 2020

Rais wa Iran Hassan Rouhani ameupinga mswada ulioidhinishwa bungeni ambao ungesitisha ukaguzi wa vinu vya nyuklia vya Iran na kuiruhusu kuongeza urutubishaji wa madini ya urani, akisema unaathiri juhudi za kidiplomasia zinazolenga kuurejesha mkataba wa nyuklia wa 2015 na kuviondoa vikwazo vya Marekani. 

Akizungumza katika kikao cha baraza la mawaziri, Rouhani amesema serikali yake haikubaliani na kile inachokiona kuwa ni kikwazo kwa muenendo wa shughuli za kidiplomasia. 

Vuta ni kuvute kuhusu mswada huo, ambao ulipata nguvu baada ya kuuliwa mwanasayansi wake maarufu wa nyuklia wiki iliyopita, inaonyesha upinzani uliopo kati ya Rouhani, ambaye ni kiongozi wa siasa za wastani, na wabunge wa misimamo mikali ambao wanatawala bunge na wanapendelea mbinu ya kimamabavu dhidi ya nchi za magharibi. 

Mswada huo hautarajii kuwa na manufaa yoyote, kwa sababu kiongozi wa juu kabisa wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ana kauli ya mwisho kuhusu sera zote kuu, ikiwemo mpango wa nyuklia.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *