img

Polisi yabaini jengo la kuzalisha wasichana na kuuza watoto kimagendo

December 2, 2020

Polisi nchini Nigeria jimbo la Ogun limewakamata washukiwa wawili katika jengo ambalo linatumika kushikilia wasichana na kuwatunga mimba, vilevile watoto wanaozaliwa kuuzwa kimagendo.

Msemaji wa polisi katika jimbo hilo Abimbola Oyeyemi amesema msichana aliyelaghaiwa na mmoja wa waendeshaji jengo hilo alifanikiwa kutoroka na kuripoti kisa hicho kwa polisi.

Maafisa waliovamia jengo husika walinusuru wasichana 10, wanne kati yao tayari wakiwa wajawazito, kuligana na taarifa za TVC.

Mmoja wa waliokamatwa ni msichana wa mwanamke anayesimamia jengo hilo.

Mwanamke huyo alishitakiwa kwa makosa ya ulanguzi wa binadamu na kuachiwa kwa dhamana.

Mshukiwa mwingine ni mlemavu ambaye polisi wanashuku huenda ndiye aliyewatia mimba wasichana walionusuriwa.

Maeneo kama hayo hutumika kulaghai wasichana na kuwazalisha watoto ambao huuzwa kwa njia ya magendo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *