img

Pinda: Wavuvi angalieni kesho yenu’

December 2, 2020

Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Tanzania, Mizengo Pinda amewatahadharisha wavuvi wa mikoa ya Pwani kulinda mazingira vinginevyo samaki watapotea kabisa.

 Pinda ametoa kauli hiyo leo Jumatano Desemba 2, 2020 alipoongoza kazi ya kupanda miti katika viwanja vya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jijini Dodoma.

Ametaja madhara ya ukataji wa mikoko na uvuvi wa samaki kwa kutumia mabomu, kuwa ni uharibifu mkubwa wa mazingira katika mazalia ya samaki.

Pinda amesema wavuvi wengi wanafurahia kuona wanapata samaki lakini wanasahau kesho yao na watoto wao itakuwaje.

“Uharibifu wa mazingira ni janga la dunia, hata sisi Tanzania tunapambana dhidi ya  vita hii, lakini hata wale wavuvi badala ya kuongoza mapambano wao wanashabikia, najiuliza hivi wanaijua kesho yao,” amesema Pinda.

Ametaka suala la upandaji miti liende sambamba na utunzaji wake kusudi miti istawi na kupendezesha sura ya nchi ambayo imeanza kupotea.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *