img

Mzozo wa Tigray Ethiopia: UN, Ethiopia zakubaliana kuruhusu misaada

December 2, 2020

Dakika 3 zilizopita

Msichana wa Ethiopia akiwa ameseimama kwenye foleni kupokea chakula

Umoja wa Mataifa na Ethiopia wamekubaliana kuruhusu misaada katika eneo lenye vita la Tigray, maafisa wa UN wanasema.

Msemaji wa UN Saviano Abreu amesema ujumbe wa kufanya tathmini utaanza baadaye Jumatano. Hakujakuwa na neno hadi sasa kutoka kwa serikali ya Ethiopia.

Chakula na dawa zinasemekana kuwaishia mamilioni ya watu.

Mamia ya watu wameripotiwa kuuawa katika mapigano yaliyodumu kwa mwezi mmoja kati ya jeshi la shirikisho na Chama cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF).

Serikali ya Ethiopia ilisema mji wa Mekelle ulidhibitiwa mwishoni mwa wiki.

Lakini wanajeshi wa TPLF wamesema walikuwa bado wanapigana karibu na mji.

Maelfu ya watu wamehama makazi yao.

Katika hatua nyingine, mamlaka ya Ethiopia imesema mmoja wa maafisa wakubwa zaidi TPLF amejisalimisha. Keriya Ibrahim ndiye spika wa zamani wa bunge la huko Tigray.

TPLF haijasema chochote kuhusu suala hilo.

UN na Ethiopia zimekubaliana masuala gani?

Umoja wa Mataifa utakuwa upatikanaji wa bila kikwazo wa misaada kaika maeneo yanayoshikiliwa na serikali ya Tigray, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia misaada ya kibinadamu Saviano Abreu amenukuliwa na shirika la habari la Associated Press akisema ujumbe wa kwanza wa kufanya tathmini ya mahitaji unaanza Jumatano baada ya kutiwa saini kwa makubaliano wiki hii.

“Kwa kweli tunafanya kazi kuhakikisha kuwa msaada utatolewa katika eneo lote na kwa kila mtu anayehitaji,” Bwana Abreu amesema.

Hatahivyo, serikali huko Addis Ababa bado haijathibitisha kama mpango huo umefikiwa.

1px transparent line

Kwanini serikali na TPLF zinapigana?

TPLF ilitawala maisha ya kijeshi na kisiasa ya Ethiopia kwa miongo kadhaa kabla ya Bw Abiy kuanza kazi mnamo 2018 na kushinikiza mageuzi makubwa.

Mwaka jana, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alivunja muungano unaotawala, ulioundwa na vyama kadhaa vya kikanda na kikabila, na kuwaunganisha katika chama kimoja, kitaifa, ambacho TPLF ilikataa kujiunga.

1px transparent line

Mzozo ulishika kasi mwezi Septemba, wakati Tigray ilipofanya uchaguzi, ikikaidi marufuku ya kitaifa kuahirisha uchaguzi kutokana na janga la virusi vya corona. Bwana Abiy alijibu kwa kuita kura hiyo kuwa batili.

Utawala wa Tigray unaona mageuzi ya Bwana Abiy kama jaribio la kuipatia serikali yake kuu nguvu zaidi na kudhoofisha majimbo.

Vikosi maalumu vya Tigray

Bw. Abiy alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2019 kwa jitihada zake za kuipatia amani Eritrea.

Waziri mkuu anaamini maafisa wa TPLF wanadhoofisha mamlaka yake.

Presentational grey line

Mambo matano kuhusu Tigray:

1. Ufalme wa Aksum uko katika eneo hilo. Ilielezewa kama moja ya ustaarabu mkubwa wa ulimwengu wa zamani, wakati mmoja ilikuwa serikali yenye nguvu kati ya milki za Kirumi na Uajemi.

2. Magofu ya mji wa Aksum yametambuliwa na Umoja wa Mataifa kama eneo la turathi za kale duniani. Eneo hilo ambalo limekuwepo kati ya karne ya kwanza hadi ya tatu AD, linajumuisha , makasri, makaburi ya wafalme na kanisa linaloaminiwa na baadhi ya watu kuwa sanduku la agano (Ark of the Covenant).

Aksum unaaminika kuwa makazi ya malkia wa sheba

3. Watu wengi katika eneo la Tigray ni Wakristo wa dhehebu la Orthodox Ethiopia. Mzizi wa Dini ya Kikristo ulianza kuchipuka miaka 1,600 iliyopita.

4. Lugha kuu katika eneo hilo ni Tigrinya, lahaja ya Kisemeti ina wasemaji wasiopungua milioni saba ulimwenguni.

5. Ufuta ni zao kuu la biashara, unasafirishwa Marekani, China na nchi nyingine.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *