img

Msimamo wa Qatar wa kuunga mkono Palestina

December 2, 2020

Qatar imetangaza kushikilia msimamo wake ambao haujabadilika katika suala la kuunga mkono Palestina.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Muhammed bin Abdurrahman Al Sani, aliandika ujumbe kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii katika Siku ya Kimataifa ya Mshikamano wa  Wapalestina na kusema,

“Katika Siku ya Kimataifa ya Mshikamano  wa Wapalestina, tunasisitiza kushikilia msimamo wetu kama Qatar, na tunaunga mkono suala la ndugu zetu wa Palestina kupewa haki yao ya kuunda taifa lao huru la kujitegemea ambalo mji mkuu wake ni Jerusalem.”

Ikiwa ni pamoja na uamuzi uliochukuliwa kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mnamo tarehe 29 Novemba 1977,  tarehe 29 imekuwa ikiadhimishwa kila mwaka tangu 1978 kama “Siku ya Siku ya Kimataifa ya Mshikamano  wa Wapalestina ” ili kuunga mkono suluhisho la mzozo wa Palestina.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *