img

Mjerumani aliyegonga kundi la watu na kuwauwa 5 azungumza na polisi

December 2, 2020

Polisi nchini Ujerumani imesema leo kuwa mtu aliyeliendesha gari lake kiholela kwa mwendo wa kasi na kuingia eneo la watu wanaotembea kwa mguu katika mji wa kusini magharibi mwa Ujerumani Trier, ameanza kuzungumza na wapelelezi. 

Tukio hilo la jana lilisababisha vifo vya watu watano akiwemo mtoto mdogo wa miezi tisa na kuwajeruhi vibaya wengine kadhaa. Maafisa hawajatoa maelezo zaidi kuhusu kile ambacho mshukiwa huyo anawaambia polisi. 

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 51 mzaliwa wa eneo hilo la Trier, alikamatwa katika eneo la tukio hilo jana. 

Vyombo vya habari Ujerumani vimeripoti kuwa alitarajiwa pia kufanyiwa uchunguzi wa kiakili. Maafisa wamesema hakukuwa na ishara yoyote kuwa kulikuwa na nia yoyote ya kigaidi, kisiasa au kidini ambayo ilichangia.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *