img

Je Zinedine Zidane kubwaga manyanga Real Madrid ?

December 2, 2020

Kocha wa klabu ya Real Madrid ya Hispania, Zinedine Zidane amesema hatojiuzulu nafasi yake licha ya kipigo ilichokipokea jana dhidi ya Shaktar Donetsk cha bao 2-
0 kilichohatarisha nafasi ya mabingwa hao wa kihistoria kufuzu hatua ya 16 bora ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Zidane amesema kwamba kikosi chake kina nafasi ya kufuzu katika mchezo wa mwisho ambao utawalazimu wawanyuke vinara wa kundi B, Borussia Monchegladbach ambao katika mchezo wa mkondo wa kwanza walitoka sare ya bao 2-2.

Raia huyo wa Ufaransa amesema anauwezo wa kubadili hali iliyopo hivi sasa ingawa watapitia changamoto kubwa lakini anaimani watavuka hatua inayofuata.

Real Madrid ilipokea kipigo cha pili kutoka kwa Shaktar Donetsk, huku Inter Milan ikiitandika Monchegladbach bao 3-1 na kulifanya kundi hilo kuwa wazi kwa timu zote nne kufuzu hatua ya 16 bora.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *