img

Hong Kong : Fahamu mji huu unaopenda ushirikina zaidi duniani na vituko vyake

December 2, 2020

Dakika 3 zilizopita

Feng Shui

Wakati wa siku ya joto na baridi mjini Hong Kong, mfanyikazi wa masuala ya kifedha katika mji huo Wai Li hutembelea Wong Tai Sin, hekalu lenye shughuli nyingi jijini, ili kufanya shughuli ya kutabiri kwa jina kau cim.

Nadhani raia wengi wa Hong Kong wanapendelea ushirikina kwa njia moja au nyengine. Wengi hutumia ushirikina kuongeza bahati yao ama kuzuia bahati mbaya.

Shughuli hiyo maarufu inashirikisha kutikisa bomba lenye vijiti 100 vya mianzi hadi kijiti kimoja kitakapoanguka chini. Kila kijiti kina hadithi inayolingana ambayo ikitafsiriwa na wafanyakazi watabiri wa hekalu hilo inatoa fursa ya kujua hali yako ya baadaye.

Li anapiga magoti juu ya mto wa maombi mbele ya madhabahu ya hekalu hilo, anafunga macho yake na kuanza kutikisa bomba la vijiti 20 vya bahati huku akizingatia swali ambalo anataka lijibiwe. Dakika chache baadaye Vijiti 24 vinaanguka chini.

Na baadaye akielekea katika eneo la hekalu hilo linalotabiri bahati , Li anakutana na Mwalimu Joseph, mtabiri mkongwe wa miaka 20, ambaye hufanya tafsiri kwa kutumia muongozo wa fimbo yake .

Wong Tai Sin is a Chinese Taoist deity popular in Hong Kong (Credit: Credit: Bushton3/Getty Images)

Akiketi mbali naye kwenye kibanda chake, Mwalimu Joseph anamwambia Li asitarajie maendeleo yoyote au kupandishwa vyeo mwaka huu na kwamba atapata shida chache mbele ya kazi. Kwa ujumla, anasema, bahati yake itakuwa wastani..

Li, ambaye alitembelea hekalu hilo mara kadhaa siku za nyuma, anaamini usomaji huo ni sahihi. “Wong Tai Sin hajawahi kunikosea hapo awali,” alisema. “Siku zote huwa ninakuja hapa wakati wowote nina maswali au maamuzi ya kufanya juu ya maisha yangu ya baadaye. Ninahisi ni sahihi;”

Li sio mtu anayefuata dini lakini, kama wengi wa wageni 10,000 wa kila siku ambao hupitia hekalu hilo, yeye ni mtu huru linapojiri suala la ushirikina . “Ikiwa mimi ni mwaminifu, nadhani watu wengi wa Hong Kong wanafanya ushirikina kwa njia fulani. Watu wengi hapa watafanya vitu ili kuongeza bahati zao au kuepusha bahati mbaya. “

Ilikuwa ushirikina, Li anasema, ambao ulimzuia kukodisha ghorofa mpya hivi karibuni. “Usimamizi wa jengo hilo ulinipa chumba 1404,” alisema Li. “Sikuweza hata kutazama ghorofa hiyo kwasababu nambari ya nyumba niliopewa nilihisi kana kwamba itaniuwa “. Sitaki kujihatarisha kuishi huko, ingawa walinipa punguzo kubwa la kodi. “

Li hayupo pekee katika kuzuia au kuogopa chochote kinachohusiana na nambari nne, kitu ambacho kinajulikana kama “tetraphobia”. Inaaminika kwamba nambari nne ni sawa na kifo. Nambari kumi na nne na 24 zinachukuliwa kuwa mbaya zaidi, kwasababu nambari 14 inaaminika kuwa utakufa huku nambari 24 ikiaminiwa kuwa ni “rahisi kufa”. Majengo ya vyumba, hoteli, ofisi na hata hospitali katika jiji mara nyingi huruka ghorofa zilizo na nambari hizo.

“Ni jambo la ushirikina,” alisema John Choi, ambaye amefanya kazi kama bwana feng shui huko Hong Kong kwa zaidi ya miaka 10. “Hata kwenye jengo langu la ghorofa ya 40 hadi 49 hazipo. Inaisha na 39 halafu huendelea na ghorofa ya 50 . Halafu hakuna ghorofa ya 4, ghorofa ya 14, 24 au gorofa ya 54.

Mbali na ukosefu wa ghorofa zenye nambari nne, muonekano mwingine wa kawaida nje ya majengo na nyumba kote jijini humo ni makaburi ya Tu Di Gong. Kawaida makaburi hayo yapo nje ya lango kuu la majengo, makaburi haya ni ya mungu wa Wachina Tudi Gong, Mungu wa Udongo na Ardhi, ambaye anaaminika kuweka mbali nguvu hasi au vizuka, na kuwabariki watu wanaoishi kwenye uwanja wake.

“Watu wengi hapa wanaamini miungu na roho zina nguvu kubwa ya kubadilisha bahati au hatma ya mtu,” alisema Choi. “Unaweza kupata maduka mengi yana kaburi la Tu Di Gong lililoko karibu na mlango wao mkuu. Kwa maana hiyo hiyo, ni kama ofisi ya usimamizi inayowazuia waingiliaji kuingia kwenye duka. “

Choi anasema kuwa hali ya ushindani mkali uliopo jijini humo ndio unasababisha watu wengi kutumia imani za ushirikina kujaribu kukuza bahati na fursa zao.

“Katika eneo lenye ushindani mkubwa, unawezaje kuwashinda wengine?” Aliuliza Choi. “Kitu pekee unachoweza kufanya ni kumtumia feng shui kusaidia kuongeza bahati yako

Feng Shui, haswa “upepo na maji”, ni mazoezi ya zamani ya Wachina ya kutumia nguvu za nishati kuoanisha watu binafsi na mazingira yao ya karibu ili kuleta bahati nzuri na afya. Aina ya utafitii (mazoezi ya kupanga au kuweka majengo au tovuti zingine kwa bahati nzuri), leo imepigwa marufuku katika bara la China na Chama cha Kikomunisti kama “ushirikina wa kimwinyi”, kwani unaenda kinyume na imani kuu ya chama cha taifa hilo .

“Wakati walipopiga marufuku feng shui nchini China, Washiriki wengi wa feng shui walikimbia na kuja Hong Kong,” alisema Choi. “Baadhi yao pia walikwenda Taiwan kwa sababu zile zile.”

Leo, feng shui inabaki maarufu huko Hong Kong, na Choi anasema karibu 40% ya watengenezaji wa jengo bado wanashauriana na bwana wa feng shui kushauri juu ya muundo mzuri zaidi wa miradi yao. Bei za mashauriano kawaida huanzia HK $ 8 / sq ft na bwana wa kawaida, hadi HK $ 30 / sq ft na bwana wa kiwango cha juu. Ikiwa ni mradi mpya wa ujenzi, inaweza kuanzia HK $ 1m hadi dola milioni chache kwa kila mradi.

Katika eneo lenye ushindani mkubwa, unawezaje kuwashinda wengine? Kitu pekee unachoweza kufanya ni kutumia feng shui kusaidia kuongeza bahati yako

Majumba mengi marefu katika eneo kuu la kibiashara jijini hujulikana kama majengo ya feng shui. Kwa kweli, sifa zao nyingi za muundo zinashawishiwa itikadi za zamani na Fengshui.

Wataalam wanasema kuna vita vya feng shui vinavyotokea katikati mwa jiji. Jumba refu la Benki Kuu ya China inasemekana linafanana na kijembe ambacho kinakata utajiri wa majengo yanayolizunguka kwa kutumia nishati yake inayojulikana kama “sha qi”, ambayo inamaanisha “kuua nishati”. Jengo la jirani la HSBC linadaiwa kuongeza vitu viwili kama mizinga (winchi za huduma) juu ya paa lake kama kinga.

Muda mfupi baada ya jumba refu la Benki kuu ya China kukamilika mnamo 1989, bei ya hisa za HSBC zilipungua katika historia yake. Ili kukabiliana na nishati hasi, HSBC inasemekana ilielekeza vitu vyake kama kanuni moja kwa moja kwenye Benki ya China. Tangu wakati huo, kulingana na hadithi, utendaji wa HSBC umeboreka.

At Wong Tai Sin Temple, golden bells are labelled with the names of worshippers (Credit: Credit: Cheryl Chan/Getty Images)

At Wong Tai Sin Temple, golden bells are labelled with the names of worshippers who pray for blessings (Credit: Cheryl Chan/Getty Images)

Baada ya mashauriano marefu na wataalam wa feng shui, HSBC pia iliweka simba wawili wa shaba moja kwa moja mbele ya mlango wake mkuu. Katika feng shui, simba ni ishara ya ulinzi na utajiri na hadhi ya kijamii. Kwa kuwa HSBC ni benki ya sita kwa ukubwa ulimwenguni, baadhi ya wenyeji wanapenda kushika pua na vidole vya simba kwa matumaini kwamba utajiri wao mzuri wa feng shui utawapatia bahati.

“Tunaamini kugusa vitu vya feng shui kunaweza kuleta bahati nzuri,” alisema Choi. Ni sawa, anasema, kukaa na watu wenye bahati – utajikuta ukipata fursa nzuri zaidi, lakini hakuna dhamana yoyote. “Ili kufikia mafanikio, kuna msemo wa zamani wa Wachina ambao unasema 70% inategemea bidii yako, 30% inategemea bahati yako.”

Imani za kishirikina huko Hong Kong pia zinaelekezwa kwa marehemu. Wakati wa sherehe za kuheshimu na kuabudu mababu waliokufa, miongoni mwao siku ya kufagia kaburi inayojulikana kama tamasha la Qingming inayofanyika mwezi Aprili, waombolezaji huchoma picha za pesa, nguo, nyumba na hata vifaa vya hivi karibuni kama simu za rununu na Runinga. Inaaminika matoleo haya yatawawezesha marehemu kuwa na maisha ya baadaye yenye furaha na mafanikio.

Kwa kuwa watu hawawezi kuwa na udhibiti kamili wa maisha yao, imani za kishirikina zitakaa kwa muda mrefu kama tunaweza kufikiria

“Tunaamini kwamba ikiwa utawatunza mababu zako watakubariki ,” alisema Choi. “Baba yangu alipokufa alikuwa maskini kabisa wakati huo. Kwa hivyo tulimchomea vitu vingi ili apate kuwa tajiri katika maisha yake ya baadae. Hata mimi nilifanya hivyo. Hii ni jamii ya ushirikina baada ya yote. “

Sababu za kuwepo kwa utajiri wa imani za ushirikina Hong Kong ni ni vigumu kubaini. Baada ya kuwa chini ya koloni ya Uingereza kwa zaidi ya miaka 150 na kuchukua imani za Mashariki na Magharibi, leo wakazi wengi wanaamini ushirikina kutoka kwa tamaduni zote mbili. Kwa mfano, Wakaazi wa Hong Kong wataepuka kutembea chini ya ngazi (inachukuliwa kuwa bahati mbaya Magharibi) na vile vile kupeana saa kama zawadi (inachukuliwa kuwa bahati mbaya kwa Wachina, kwani neno saa linasikika sawa na kuhudhuria mazishi ).

Yan Zhang, profesa katika Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Singapore ambaye ameandika tafiti juu ya jukumu la mila za ushirikina katika kuzuia bahati mbaya, anasema sababu maarufu zaidi kwa nini watu wanaamini ushirikina ni kupata hisia ya kudhibiti mazingira yao

“Kufanya vitendo vya ushirikina hufanya watu kuhisi hali ya udhibiti, ambayo huwafanya wasisikie wasiwasi au woga,” alisema Zhang. “Sayansi za kidini na a ushirikina zinaweza kusaidia watu kuhisi udhibiti na faraja. Hong Kong sio mahali pa kidini, kwa hivyo ili kujisikia bora, mtu anahitaji kutegemea sayansi au ushirikina. “

Lakini kivyovyote vile , imani ya ushirikina ya jiji hilo haiwezekani kutoweka hivi karibuni. “Imani za kishirikina zinaweza kusasishwa baada ya muda wakati watu wanajua vizuri jinsi vitu fulani hufanya kazi,” alisema Zhang. “Walakini, sitarajii imani za kishirikina zitaondoka kabisa. Kwa kuwa hawawezi kuwa na udhibiti kamili wa maisha yao, imani za kishirikina zitasalia kwa muda mrefu sana.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *