img

HIMSO watoa pikipiki 4 Songwe kuaidia elimu kuhusu bima ya Afya

December 2, 2020

Na Baraka Messa , Songwe

MKOA wa Songwe umepokea pikipiki nne (4) kutoka Shirika la HIMSO ambao ni wadau wakubwa wa wa Mfuko wa huduma za jamii  (CHF) iliyoboreshwa ili kusaidia utoaji wa elimu kwa Wananchi kuhusu Mfuko wa huduma za jamii Pamoja na bima za afya.

Akikabidhi pikipiki hizo kwa Katibu Tawala wa mkoa wa Songwe Self Shekalage  Mwenyekiti wa Bodi ya HIMSO Charles Mbwanji alisema pikipiki hizo nne zina thamani ya shilingi milioni 27.1, na kudai kuwa pikipiki hizo zitagawiwa kwa Waratibu wa Mfuko katika Halmashauri zote nne za mkoa wa Songwe ambazo ni Mbozi ,Ileje , Momba na Songwe.

Alisema lengo la kugawa pikiki hizo ni kuhakikisha zinatumika kutatua changamoto mbalimbali kuhusiana na Mfuko wa jamii (CHF) ili Wananchi wazidi kunufaika.

“Tunaomba pikipiki hizi zikatumike vizuri katika maeneo muhimu katika Halmashauri zetu, tunaamini hazitatumika kwenye mambo mengine ili wananchi waweze kunufaika kwa kupata elimu muhimu” alisema Mbwanji.

Katibu tawala mkoa wa songwe self shekalage Baada ya kupokea pikipiki kutoka Shirika la HIMSO alisema  pikipiki hizo atawakabidhi wahusika , mpaka pale watakapokamilisha malengo ya kazi watakazopangiwa  na kudai kuwa atayekidhi mbapo amesema kwa sasa hatowakabidhi wahusika pikipiki hizo mpaka pale watakapokamilisha vigezo muhimu.

“Kwa sasa pikipiki zitakaa ofsini  kwangu kwa muda wa wiki moja, atakayetimiza vigezo muhimu ndiye atakabidhiwa mapema zaidi.” Alisema

Shekalage aliwanyoshea Kidole Waratibu na waandikishaji wananchi katika mfuko wa Bima ya Afya ya jamii (CHF) mkoa wa Songwe,  kwa kushindwa kufanikisha na kutatua changamoto zinazowakumba Wananchi.

 alisema shughuli ya uandikishaji wanufaika iko nyuma ya lengo la kitaifa ambapo mkoa unapaswa kufikisha walau asilimia 30 lakini hadi sasa uko nyuma kwa kuwa na asilimia 1.6

Katibu tawala aliongeza kuwa hadi sasa mkoa wa Songwe upo katika nafasi ya 24 kati ya mikoa 26 ya tanzania bara hali ambayo haimfurahisi hata kidogo, na ameahidi kuhakikisha anaandaa mkakati mzuri wa kuhakikisha hadi mwakani mkoa unapanda na kuwa na rekodi nzuri katika kusimamia mfuko huo wa (CHF) iliyoboreshwa.

Mratibu wa mfuko wa Bima ya Afya (CHF) mkoani hapa Atu Dzombe aliweka wazi kuwa hadi sasa ni jumla ya kaya 6970 zilizosajiriwa kati ya kaya 25900 zilizokusudiwa, ambapo zaidi ya nusu ya wanachama wa mfuko huo hawajahuisha unufaika wao na kuacha wanufaika 3814 ndio walio hai hadi sasa.

Alisema tatizo linalosababisha wanachama wa CHF kutojiunga ni uelewa mdogo wa CHF ya zamani ambayo walikuwa wanachangia Sh.10000 na CHF iliyoboreshwa ambayo mchangiaji anapaswa kuchangia Sh.30000

” tofauti yake inatokana na aina ya kifurushi anachopata mwanachama CHF ya zamani mwanachama alikuwa anapata kifulushi kimoja yaani anatibiwa katika wilaya alikojiandikisha, lakini hii iliyoboreshwa kifurushi chake mwanachama anatibiwa kufikia ngazi ya mkoa nchi nzima na wategemezi wake” alisema Dzombe.

Aliongeza kuwa hivi sasa jitihada zinafanywa kutoa elimu kwa wananchi ili waelewe faida za CHF iliyoboreshwa.

Baadhi ya wananchi wakazi wa Vwawa waliohojiwa na gazeti hili Isaya Mwabulambo na Joyce Mwamlima walisema sababu za watu kutoitikia kujiunga na mfuko wa bima ya afya kuwa ni kitendo cha kukosa huduma ya dawa Mara kwa Mara wanapokwenda kupata matibabu katika vituo vya tiba na hospitali.

” Seriikali iangalie upya vituo vya tiba Mara nyingi vinakosa dawa tukienda kutibiwa tunaambiwa tukanunue dawa kitendo ambacho hatuoni umuhimu wa kuwa na bima” alisema Mwabulambo.

Joyce Mwamlima alisema sababu nyingine inayokatisha tamaa ni pamoja na uelewa mdogo kuhusu masuala ya bima za afya na umasikini wa kipato ambapo mtu anaona ugumu wa kuchangia mapema matibabu.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *