img

Emmanuel Okwi kurejea tena ndani ya Simba

December 2, 2020

 

IMEELEZWA kuwa Emmanuel Okwi anaweza kurejea tena ndani ya Klabu ya Simba ili kuendeleza huduma yake kikosini hapo kutokana na safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kusumbuliwa na majeraha

John Bocco mwenye mabao saba, Meddie Kagere mwenye mabao manne na Chris Mugalu mwenye mabao matatu hawa ni chaguo la kwanza la Sven Vandenbroeck lakini wamekuwa wakikosekana kwenye baadhi ya michezo kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Plateau United uliochezwa Uwanja wa New Jos nchini Nigeria, Bocco alianza na Kagere hakuweza kucheza kutokana na kukosa mechi fitnes.

Alishuhudia timu yake ikishinda bao 1-0 ugenini kupitia kwa Clatous Chama akiwa benchi.

Habari zimeeleza kuwa kutokana na mipango ya Simba kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika imeweka mpango wa kumrejesha Okwi ambaye ana maelewano mazuri na Clatous Chama, Meddie Kagere, John Bocco na Mohamed Hussein kwa kuwa alishacheza nao msimu wa 2018/19.

“Okwi bado yupo kwenye hesabu za Simba na wakati ukifika anaweza kurejea kikosini hivyo ni jambo la kusubiri na kuona kwani hata kwenye usajili wa dirisha kubwa alikuwa kwenye hesabu ila mambo yalikwama.” ilieleza taarifa hiyo

Msimu uliopita, Okwi aliweka ujumbe wa pongezi kwa Simba baada ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara na kumuambia Chama kuwa anaamini wataonana hivi karibuni.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ameweka wazi kwamba kwenye suala la usajili wataangalia ripoti ya mwalimu inasema nini kisha watashusha majembe ya kazi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *