img

Afghanistan, Taliban wakubaliana kuendelea na mazungumzo ya amani

December 2, 2020

Wawakilishi wa serikali ya Afghanistan na Taliban wamesema leo kuwa wamefikia makubaliano ya awali ya kuendelea na mazungumzo ya amani. 

Makubaliano hayo ya kwanza kutiwa saini na pande mbili katika miaka 19 ya vita yamepongezwa na Umoja wa Mataifa na Marekani. Muafaka huo unaweka muongozo wa mashauriano zaidi na unazingatiwa kuwa hatua kubwa kwa sababu utawaruhusu wajumbe kusonga mbele na masuala mazito zaidi yakiwemo mazungumzo ya kusitisha mapigano. 

Mwanachama wa timu ya wajumbe wa serikali ya Afghanistan Nader Nadery amesema utaratibu wa mazungumzo hayo umekamilika na sasa yataendelea kuanzia sasa. Msemaji wa Taliban pia amethibitisha makubaliano hayo kwenye mtandao wa kijamii Twitter. 

Muafaka huo unakuja baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo mjini Doha yakihimizwa na Marekani. Nchini Afghanistan, pande zote mbili bado zipo vitani, huku mashambulizi ya Taliban dhidi ya vikosi vya serikali yakiendelea bila kuzuiwa.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *