img

Watumishi watakiwa kufanya kazi kwa kujituma

December 1, 2020

Na Hamisi Nasri,Masasi 

   MBUNGE wa jimbo la Masasi mjini,Geofrey Mwambe amezitaka sekta za elimu,afya,maji na nishati wilayani Masasi mkoani Mtwara kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake wajikite katika kutimiza majukumu yao kwa uadilifu na kujituma zaidi ili kuweza kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta hizo.

    Mwambe Aliyasema hayo jana mjini Masasi na mbunge wa jimbo la Masasi mjini,Geofrey Mwambe alipokuwa akizungumza na watumishi wa sekta hizo kwa nyakati tofauti wakati wa ziara yake ya kikazi kwenye sekta ya afya, elimu na nishati,katika ziara hiyo mbunge aliambatana na wazee maarufu, madiwani wateule na viongozi mbalimbali wa serikali.

     Awali akizungumza na watumishi wa shirika la umeme wilaya ya Masasi (Tanesco) Mwambe alisema kuwa akiwa kama mbunge wa Masasi atahakikisha huduma ya umeme ikiwemo umeme vijijini unaowafikia wananchi wengi zaidi katika vijiji vyao.

    Alisema angependa kuona watumishi hao wa Tanesco wanafanya kazi kwa uweledi zaidi na kwa kujituma katika utoaji huduma ya nishati kwa jamii na pale wanapokwama basi wawe wepesi kutoa taarifa ofisi ya mbunge ili kwa pamoja kuweza kutatua changamoto zinazojitokeza.

   Mwambe alisema amesikitishwa kuona umeme wa REA bado vijiji vyingi katika jimbo la Masasi bado havijaunganishiwa umeme hivyo wahusika waone umuhimu wa kulishugulikia jambo hilo na vijiji hivyo viweze kupata umeme,ofisi ya mbunge pia iltafuatilia jambo hilo kuona linafanyiwa kazi.

    Aidha, Mwambe alikutana na watumishi wa shule ya sekondari ya kutwa Masasi, watumishi na wanachuo wa chuo cha afya na sayansi shirikishi( COHAS) wilayni Masasi alisema katika ziara yake hiyo amebaini changamoto kadhaa kwa watumishi na miundombinu iliyopo kwenye sekta hizo ikiwemo uchakavu majengo.

   Alisema akiwa kama mbunge atahitaji kupewa ushirikiano wa karibu kutoka kwa watumishi hao ili kwa pamoja kuweza kupambana katika kuona sekta hizo zikiondokana na changamoto hizo na kwamba zikiweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi ambao utaleta tija kwa wananchi wa jimbo hilo.

 “Mimi hata kabla ya kuwa mbunge huko nilikotoka kwenye taasisi nilizowai kuzifanyia kazi nimekuwa ni mtu ambaye napenda sana ufanyaji kazi wa kujituma na kiwango kinachotakiwa hivyo naomba watumishi tufanya kazi kwa bidii ili kuleta tija ya kile tunachokifanya, alisema Mwambe akiwa na watumishi wa sekondari hiyo ya kutwa Masasi.

   Alisema kupitia ziara yake hiyo kwenye sekta hizo amejifunza kitu kizuri na kwamba ni jambo la msingi ambalo anajenga matumaininalo ni watumishi wa sekta hizo kufanya kazi zao za kutoa huduma kwa wananchi kwa kiwango kilichotukuka ili kila mwananchi aweze kufuarahia huduma zinazotolewa na sekta hizo.

    Kwa upande wake meneja wa shirika la umeme wilayani Masasi,Kidara Maeda alisema shirikika hilo linampongeza mbunge huyo kwa kufanya ziara kwenye taasisi hiyo kwa ajili ya kusikiliza kero zilizopo na kero zilizopo ambazo ni kukatikakatika kwa umeme ambapo shirika bado linaendelea kuzifanyia kazi.

   Alisema ili kuona wananchi wa wilaya ya Masasi wanapata huduma ya umeme yenye uhakika serikali imenunua kifaa maalumu cha kuongeza nguvu ya umeme na kukifunga wilayani Masasi chenye thamani ya sh.  zaidi ya Milioni 300 jambo kimesaidia kuufanya umeme kupatikanika kwa uhakika.

   Naye mwalimu mkuu wa shule ya kutwa Masasi, Omari Kanyimbi alisema kuwa shule yake inakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa miundombinu ya majengo na upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi hivyo mbunge aone umuhimu wa kusiadia na kulisemea jambo hilo katika mbunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *