img

Watumiaji maji bonde la Wami Ruvu kusajiliwa

December 1, 2020

Bodi ya Maji ya Bonde la Wami Ruvu imeanza shughuli ya kuwatambua wanaotumia maji kwa kuwasajili ili ifikapo Februari, 2021 iwe na takwimu sahihi za watumiaji.

Ofisa wa  maji wa  bonde hilo, Simon Ngonyani leo Jumanne Desemba mosi, 2020 amesema tayari wamekubaliana na Shirikisho la watu wenye Viwanda (CTI), kampuni na taasisi mbalimbali kufunga mita ili kupata kiwango sahihi cha maji yanayotumika.

“Kwa kuanzia zoezi hili la kufunga mita litaanza kwa wadau wenye viwanda, hii yote ni katika kujua matumizi halisi ya maji hapa nchini ili itusaidie kupanga mipango ya watumiaji Maji mazuri,” amesema Ngonyani

Ngonyani amesema kuna baadhi ya kampuni ambazo si waaminifu na wanafanya udanganyifu ili wasilipe bili ya maji stahiki.

“Naomba niwakumbushe Watanzania wenzangu kuhusu sheria ya usimamizi wa rasilimali maji namba 11 ambayo inasema ulipaji wa ada za matumizi mbalimbali ya maji ni takwa la kisheria.”

“Sheria ya Maji ya mwaka 2009 Kifungu cha 43 (1) kinamtaka mtu yoyote anayetaka kuchepusha maji, kukinga, kuhifadhi, kuchukua na kutumia maji kutoka kwenye chanzo cha maji juu ya ardhi au chini au kujenga miundombinu yoyote lazima aombe kibali cha kutumia maji,” amesema.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *