img

Watu wawili wauawa baada ya gari kuwagonga wapita njia Ujerumani

December 1, 2020

Watu wawili wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kugongwa na gari lililovamia la wanaotembea kwa mguu katika mji wa kusini magharibi mwa Ujerumani, Trier. Polisi imesema dereva wa gari hilo amekamatwa ili kuhojiwa. 

Msemaji wa polisi Uwe Konz amesema bado hakuna habari za kina kuhusu kilichotokea, na kuongeza kuwa chanzo cha tukio hilo kinachunguzwa. 

Lakini meya wa Trier Wolfram Liebe amenukuliwa na televisheni ya eneo hilo akisema kuwa dereva aliliendesha gari kiholela na kuwagonga watu hao huku wengine 15 wakijeruhiwa. 

Ijapokuwa tukio hilo halijatihibitishwa kuwa shambulizi la kigaidi, limeleta kumbukumbu za mwaka wa 2016 wakati mtu mmoja alipoliendesha gari lake kiholela kwenye soko la Krismasi mjini Berlin na kuwauwa watu 12.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *