img

Wanafunzi 22 na mwalimu 1 wapigwa radi Songea

December 1, 2020

Wanafunzi 22 na mwalimu mmoja wa shule ya msingi De Paul iliyopo kata ya Msamala Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, wamepigwa na radi leo Desemba 1, 2020.

RPC wa Ruvuma Simon Marwa amesema wanafunzi hao pamoja na mwalimu, wamepata mshtuko mkubwa na kukimbizwa hospitali ya mkoa huo kwa ajili ya kupata matibabu.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Songea, Pololety Komando Mgema, amewataka wazazi kuwa makini na watoto hasa kipindi hiki ambacho mvua zinanyesha na kuambatana na radi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *