img

Wafungwa 8 wafariki kwenye ghasia zilizozuka ndani ya gereza la Mahara nchini Sri Lanka

December 1, 2020

Wafungwa 8 wameripotiwa kupoteza maisha na wengine 45 kujeruhiwa kufuatia ghasia zilizozuka ndani ya gereza moja lenye ulinzi mkali lililoko katika Jimbo la Magharibi mwa Sri Lanka.

Msemaji wa Idara ya Usalama Ajith Rohana,  alieleza kuwa wafungwa wa gereza la Mahara lenye ulinzi mkali lililoko umbali wa kilomita 15 kaskazini mwa mji mkuu wa Colombo, walisababisha ghasia na vurugu ndani.

Akifahamisha kuwa mamia ya wafungwa walijaribu kudhibiti hali ya gereza na kutoroka, Rohana alisema walinzi walifyatua risasi ili kukabiliana nao.

Rohana aliongezea kusema kuwa wafungwa 8 walipoteza maisha na wengine 45 kujeruhiwa kwenye ghasia zilizotokea ndani ya gereza la Mahara, ambalo ni moja ya magereza yenye wafungwa wengi zaidi nchini humo.

Wafungwa wengi pamoja na walinzi 2 wanaarifiwa kuwa kwenye hali mbaya, na vikosi vingi vya usalama vimepelekwa kwenye gereza hilo ili kudhibiti hali ya usalama.

Kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya ndani, wafungwa hao walipinga ongezeko la kesi za maambukizi ya  virusi vya corona (Covid-19) gerezani, kudai waachiliwe mapema kwa dhamana na kutaka hali iboreshwe.

Wafungwa zaidi ya 2 wamepoteza maisha kwa covid-19 na wengine zaidi ya elfu moja kukutwa na kezi za maambukizi ya kwenye magereza 5 yenye idadi kubwa ya wafungwa katika miji tofauti ya nchi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *