img

Tetesi za soka Ulaya Jumanne 01.12.2020: Giroud, Torres, Ferrari, Schuurs, Eriksen, Alaba.

December 1, 2020

Dakika 8 zilizopita

chesea

Inter Milan wanataka kumleta mshambuliaji Mfaransa kutoka Chelsea Olivier Giroud, 34, kwa mkataba wa mkopo wa miezi sita mwezi Januari, wakiwa na chaguo la kumnunua . (Tuttosport via Mail)

Lakini Inter Milan wanaweza kukabiliwa na ushindani kutoka mahasimu wa Serie Juventus, kwani meneja Andrea Pirlo anataka kuwaleta wachezaji wake mwezi Januari, akiwemo Giroud. (Ilbianconero via Calciomercato- in Italian)

Chelsea wataanzisha mazungumzo na mlinzi wa Bayern Munich David Alaba, 28, Januari wanataka kumsaini mchezaji huyo wa Austria kwa mkataba utakaomruhusu kuhama bila malipo wakati mkataba wake utakapokamilika msimu . (AS via Sun)

Eric Bailly,
Maelezo ya picha,

Eric Bailly

Manchester United wanamatumaini kwamba Villarreal wanaweza kushawishika kumchua mchezaji wao wa zamani mlinzi Muivorycoast Eric Bailly, kama sehemu ya mpango wao kumnunua kiungo wa kati-nyuma wa Uhispania Pau Torres, 23, kwa pauni milioni 60. (Team Talk)

Liverpool wataweza kusaini mkataba na mlinzi wa Ajax Perr Schuurs kama watatoa pauni milioni 27 kwa kijana huyo mwenye umri wa maika 21. (De Telegraaf via Liverpool Echo)

Tottenham wanamfuatilia kwa karibu mchezaji wa safu ya kati-nyuma Sassuolo , Gian Marco Ferrari, 28, kabla ya uwezekano wa kuhamia Italia Januari . (90min)

Manchester United wanaweza kumnunua kiungo wa kati Inter Milan Christian Eriksen, 28, kama mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark international hatatakiwa na klabu yake ya zamani Tottenham. (Football Insider)

m

Barcelona walikataa dau la euro milioni 250 (£224m) kutoka Inter Milan kwa ajili ya Muargentina Lionel Messi, 33, mwaka 2006, kulingana na rais wa zamani wa klabu hiyo Joan Laporta. (Football Italia)

Mlindalango wa Ufaransa na Fulham Alphonse Areola, 27, anasema alikataa maombi ya kujiunga na klabu kadhaa ikiwa ni pamoja na Real Madrid na Paris St-Germain kwa kuwa alipendelea kujiunga na klabu ya Primia Ligi . (Canal+ via Football London)

Uamuzi wa winga wa Rangers Ryan Kent wa kubadili mawakala katika msimu huu wa soka unaweza kumpelekea kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye alijhusishwa na klabu ya Leeds msimu uliopita kuihama , kulingana na meneja wa zamani Gers boss Alex McLeish. (Glasgow Evening Times)

m

Mchezaji wa safu ya kati Bayern Munich Javi Martinez, 32, amedokeza kuwa ataondoka klabu hiyo ya Championi Ligi ya Ujerumani wakati mkataba wake utakapoisha mwezi Juni mwaka ujao, ” kujaribu kitu kingine kipya “. (Reuters via Eurosport)

Kiungo wa kati wa AZ Alkmaar Mohamed Taabouni, 18, yuko tayari kuhamia Italia au Uhispania Januari, huku klabu kadhaa zikimfukuzia kijana huyo kutoka timu ya kimataifa ya vijana chipukizi ya Uholanzi . (Voetbal International – in Dutch)

Newcastle wanaangalia uwezekano wa kusaini mkataba wa kudumu na mchezaji wa klabu ya Ujerumani ya Eintracht Frankfurt Jetro Willems, 26 baada ya mlinzi wao Mholanzi kulazimishwa kuondoa kipengele chake cha kucheza kwa mkopo katika mkataba wake katika St James’ Park mwezi Januari kwasababu ya jeraha baya la goti . (Shields Gazette)

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *