img

Tete: Mchezaji wa Shakhtar Donetsk aliyeiadhibu Real Madrid

December 1, 2020

Dakika 9 zilizopita

Mchezaji wa Brazil na Shakhtar Donetsk Tete katika

Maelezo ya picha,

Mchezaji wa Brazil na Shakhtar Donetsk Tete katika

Ndio wakati ambapo kinda wa Shakhtar Donetsk mwenye umri wa miaka 20, Tete alijitangaza kwa dunia.

Goli zuri, usaidizi aliotoa mbali na mchezo mzuri aliouonyesha yeye binafsi ulisaidia timu hiyo ya Ukraine kuiaibisha Real Madrid katika kipindi cha kwanza cha mechi ya kombe la klabu bingwa Ulaya mwezi Oktoba ambapo mabingwa hao walichapwa magoli 3-0.

Klabu hiyo ya Ukraine ilidhibiti uongozi huo na kumaliza washindi kwa magoli 3-2 na sasa kabla ya mechi muhimu ya marudio kuchezwa siku ya Jumanne , kiungo huyo mshambuliaji wa Brazil tayari ameonesha kile ambacho huenda ni wakati muhimu wa mchezo wake.

”Mechi hiyo ya Real Madrid ndio iliokuwa bora na muhimu katika kipindi chote cha mchezo wangu” , Tete aliambia BBC Sport katika mahojiano ya kipekee.

”Ilikuwa heshima kubwa kucheza dhidi ya magwiji kama vipi Marcelo na Casemiro – ilikuwa ndoto ilioafikiwa. Nilitaka kuonyesha ujuzi wangu na kuthibitisha hivyobasi nilimchenga Marcelo tukiwa nimesalia naye”.

”Nilifurahia kuisaidia timu yangu kupata matokeo mazuri na muhimu kama hay”o.

Kiwango cha mchezo wa Tete mjini Madrid kilionesha uwezo wake kujiunga na orodha ya wachezaji nyota wa Brazil ambao walinoa vipaji vyao katika klabu ya Shakhtar kama vile Kiungo wa Manchester City Fernandinho , kiungo wa Arsenal Willian na Douglas Costa wa Juventus ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo akiichezea Bayern.

Wakiwa maarufu kwa kusaka vipaji vya wachezaji nchini Brazil, Kikosi cha Shakhtar kimekuwa kikiundwa kwa kuwategemea wachezaji wa Brazil kwa takriban miongo miwili sasa.

Kuna wachezaji 13 wa Brazil katika timu hiyo lakini hadithi ya Tete ni maalum sana.

Baada ya kusajiliwa kwa dau la £13.5m kutoka kwa klabu ya Gremio mapema 2019 bila kukichezea kikosi cha kwanza , alifurahia kujiunga na klabu hiyo akiwa mchezaji bora wa mechi katika mechi iliotoka sare 1-1 dhidi ya Manchester City mwaka mmoja uliopita.

”Haikuwa vigumu kufanya uamuzi kuhamia klabu hiyo, kwasababu nilijua mazingira yake yatakua mazuri kwangu. Nilizungumza na Douglas Costa , ambaye alikulia katika klabu ya Gremio kama mimi na akaniambia kwamba kuna wachezaji wengi wa Brazil katika klabu ya Shakhtar”, alisema.

”Haikuwa rahisi kuingiliana na klabu hiyo. Mkufunzi Luis Castro ni raia wa Ureno na hata mtaalamu wa Lishe anatoka Portugal”.

”Kila mmoja anazungumza Kireno hapa na klabu hii inafanya kila juhudi kuhakikisha kuwa tunajihisi nyumbani. Anatumai kufuata nyayo za Douglas Costa huku Ronaldinho ,pia akiwa mchezaji wa zamani wa klabu hiyo anayeenziwa sana .

Lakini Tete hupata shinikizo kubwa akiwatazama nyota wa zamani wa Brazil.

”Nampenda sana Pele”, anasema.

”Alikuwa mchezaji mzuri sana na nimekua nikitazama kanda zake za video katika simu yangu katika chumba cha maandalizi kabla ya mechi kuanza. Ingekuwa ndoto yangu kukutana naye, ama kuzungumza naye. Pengine nikiishinda Real Madrid kwa mara nyengine nitaweza kuafiia ndoto yangu”.

Tete

Tete ambaye ni shabiki mkubwa wa Barcelona , aliongezea: Ndoto yangu kubwa ni kuichezea klabu ya Barcelona. Ronaldinho, Rivaldo, Romario na Ronaldo waliichezea Barcelona na ningependa kujiunga na orodha hiyo .

”Ukweli ni kwamba ninapocheza dhidi ya Real Madrid haitaniharibia hata chembe. Pia nilikuwa nikifuatilia sana klabu ya Liverpool na Man United , na pia nazipenda sana zote licha ya kwamba ni mahasimu wakuu. Ndizo klabu kubwa nchini England”.

Akipatiwa jina la utani Furacao (Hurricane), mtindo wa Tete unafanana na mchezaji wa Chelsea wa zamani Arjen Robben, kwasababu anapenda kuingia katikati ya uwanja kwa mguu wake wa kushoto.

“Kwanza niliichezea timu ya vijana ya Gremio na waandishi wakanipatia jina hilo. Napenda kwasababu ndivyo ninavyocheza. Nilikuwa nikicheza katika kiungo cha kati wakati nikiwa kijana mdogo na nikajaribiwa upande wa kushoto mara kadhaa lakini winga wa kulia ndio nafasi yangu ninayoipenda. Watu huniambia kwamba nacheza kama Robben, na ni vyema kujaribu ili kuafikia kiwango kama chake”.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *