img

Rais Erdoğan akutana na Waziri Mkuu wa Ukraine

December 1, 2020

 

Rais Recep Tayyip Erdoğan amempokea Waziri Mkuu wa Ukraine Denys Shmyhal katika mji mkuu wa Ankara.

Shughuli ya mapokezi hayo yaliyofanyika katika Ikulu ya Rais yalidumu kwa dakika 50.

Waziri Mkuu Shmyhal aliandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii Twitter na kubainisha furaha yake kukutana na Erdoğan, na kusema kuwa Uturuki ni moja ya nchi muhimu katika kuhakikisha utulivu na usalama wa kanda ya Blacksea, na kuwa na jukumu muhimu katika suala hili.

Akibainisha kuwa Uturuki inataka kuimarisha ushirikiano wake na Ukraine Denys Shmyhal alisema,

“Makubaliano ya biashara huria yatahimiza ushirikiano huu.”

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *