img

Ngorongoro Heroes kibaruani tena baada ya kufuzu Afcon

December 1, 2020

 USHINDI walioupata jana, Ngorongoro Heroes wa bao 1-0 dhidi ya Sudani Kusini umewapa nafasi ya kutinga michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa Vijana chini ya miaka 20.(Afcon)

Bao pekee la Ngorongoro lilipatikana dakika ya 55 kupitia kwa Kassim Shaban baada ya kipa wa timu hiyo kutema mpira uliopigwa na Kelvin John.

Kesho Desemba 2 inatarajiwa kuwa fainali kati ya Ngorongoro Heroes ambao ni wenyeji dhidi ya Uganda ambao walishinda mabao 3-1 dhidi ya Kenya kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Black Rhino, Karatu.

Afcon ya vijana inatarajiwa kufanyika nchini Mauritania mwakani, ambapo kupitia michuano ya Cecafa inayoshirikisha timu za Afrika Mashariki na Kati Ngorongoro Heroes imepata tiketi hiyo.

Nahodha wa Ngorongoro Heroes, Kelvin John amesema kuwa ushindi ambao waliupata jana ni zawadi kwa mashabiki hivyo watapambana kesho kupata ushindi mbele ya Uganda kwenye hatua ya fainali.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *