img

Mwanasayansi wa Iran ‘aliuliwa kwa silaha iliyoongozwa mbali na tukio

December 1, 2020

Mkuu wa masuala ya usalama Ali Shamkhani alisema kuwa washambuliaji walikuwa “wametumia kifaa cha kielekroniki ” wakati gari la Fakhrizadeh lilipofyatuliwa mashariki mwa mji mkuu Tehran.

Alikuwa akizungumza katika mazishi ya mwanasayansi huyo ambaye Israeli ilimshutumu kwa kusaidia kisiri kutengeneza silaha za nyuklia.

Israel haijatoa kauli yoyote wazi kuhusu madai ya uhusika wake.

Iran inaamini kuwa Israel na kikundi cha upinzandi walitumia silaha ya kielektroniki (remote control)kumpiga risasi mwanasayansi wa ngazi ya juu wa nyuklia Mohsen Fakhrizadeh Ijumaa.

Iran yailaumu Israel kwa mauaji ya mwanasayansi wake wa nyuklia

Katika miaka ya 2000, Fakhrizadeh alikuwa na mchango mkubwa katika mpango wa nyuklia wa Iran, lakini mwanasayansi huyo wa serikali amekuwa akisisitiza kuwa mpango wake wa nyuklia wote ni wa amani.

Iran imekuwa ikiwekewa vikwazo na mataifa ya magharibi kwa lengo la kuizuia kutengeneza silaha zaq nyuklia.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *