img

Mdee: Hakuna aliyelipwa, sisi ni Chadema ndakindaki

December 1, 2020

“Pamoja na kwamba mimi na wenzengu tumechukuliwa hatua za kinidhamu na Kamati Kuu ya Chadema lakini niwahakikishie kuwa tutabaki kuwa wananchama wa Chadema ndakindaki, pamoja na changamoto ambazo tunapitia.

“Tuwahakikishie wanachadema nchi nzima, Halima nayemfahamu na wenzangu tutabaki vilevile, kumekuwa na maneno mengi kwamba timenunuliwa, ila mimi Mdee sijawahi kununuliwa, sitamunuliwa na sitanunuliwa, waliofanyakazi na mimi wanajua, mimi sina thamani ya kipande cha fedha,” amesema Halima Mdee kwenye Mkutano wake na Waandishi wa Habari.

Mdee pia amesema hakuna yeyote aliyepewa hela, na kama kuna mambo yoyote yaliyotokea yalikuwa na dhamira nzuri kwa chama na kwa siasa za wanawake hivyo hakuna aliyelipwa.

Pia amewataka watu wasome Zaburi 35 ambayo itawapa mambo mengi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *