img

Magenge haramu yanayowauza wanawake kingono Scotland

December 1, 2020

Dakika 3 zilizopita

Human trafficking

Magenge ya uhalifu yameendelea kuimarisha biashara ya usafirishaji wa wanawake katika Scotland na kuwalazimisha kuwa makahaba, licha ya masharti yaliyowekwa ya kudhibiti maambuki ya Covid-19 , imesema polisi ya Scotland.

Zaidi ya wanawake 80 wametambuliwa kuwa waathiriwa wa biashara hiyo haramu na kutumiwa vibaya kingono mwaka huu.

Polisi imesema kuwa vikwazo vya kusafiri na mpaka vilivyowekwa wakati huu wa janga la corona havijazuia “biashara hiyo haramu”.

Tisa kati ya waathiriwa hao walikuwa ni wasichana wenye chini ya umri wa miak 18 , mdogo zaidi kati yao akiwa na umri wa miaka 13 na mkubwa akiwa na umri wa miaka 56.

Wanawake hao 84 walihamishwa kutoka maeneo mbalimbali ya Uingereza na kutoka katika nchi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Romania, Vietnam, China na mataifa ya Afrika.

Ingawa biashara hii haramu ya usafirishaji wa wanawake kwa ajili ya kutumiwa kingono ilikuwa imepungua mwaka 2020 kiwango cha wale wanaopelekwa kwa ajili ya kutumiwa kingono kimeongozeka, kulingana rekodi za serikali ya Uingereza.

Mkuu wa polisi Sam McCluskey, na mkuu wa kitengo cha ulinzi wa rais cha polisi wa Scotland alisema: “Licha ya hatari za kiafya za Covid-19 na vikwazo vya usafiri duniani, wafanyabiashara haramu ya binadamu, wameendelea na biashara hiyo.

“Tunaamini idadi ya wanawake, na wasichana , waliotambuliwa kama waliosafirishwa kwa biashara haramu na kutumiwa vibaya kingono ni wengi kuliko inavyokadiriwa . Tunafahamu kuwa kuna waathiriwa wengi .”

‘Uhalifu unapangwa na kudhaminiwa ‘

Alisema kuwa utumiwaji vibaya wana wanawake “Unayapa magenge ya wahalifu pesa nzuri “, ambao wanaweza kutengeneza mamilioni ya pesa kwa kuwalazimisha watu kuingia katika ukahaba au katika ndoa bandia, ambazo mara nyingi hufanyiwa matangazo katika huduma za watu wa zima za mtandao.

“Watu wanaolipa pesa kwa ajili ya ngonowanapaswa kufikiria kuhusu ni nini wanakifanya ,” amesema. ” Wanaweza kuwajibika kwa kuendeleza uhalifu wa kuwatumia vibaya wanawake kwa ngonona kwa kudhamini moja kwa moja uhalifu uliopangwa .”

Alisema kuwa taarifa muhimju kuhusu unyanyasaji wa wanawake wa kingono na wafanyabiashara haramu ya usafirishaji wa wanawake mara nyingi hutoka katika jamii wanamoishi.

“Ni jukumu letu sote kutambua dalili, kuwasidia wanapotumiwa vibaya, kupinga ulanguzi wa wanawake wanaokwenda kutumiwa kwa ngono na kuzilinda jamii zetu ,” aliongeza

Kulikuwa na ongezeko kubwa katika utambuzi wa watu wenye uwezekano mkubwa wa kuwa waathiriwa wa biashara ya ngono mwaka 2019, wakati wanawake 104 waliokuwa wakisafirishwa kwa ajili ya kutumiwa kingono walipobainika.

Takwimu za wizara ya mambo ya ndani nchini Uingereza zinaonesha kuwa waathiriwa 214 waliokuwa na umri wa kati ya miaka kati ya 15 na 35 waliwasili Scotland mwaka 2019 kutoka Vietnam pekee – mwaka 2018 walikuwa ni wanawake 66.

Bronagh Andrew
Maelezo ya picha,

Bronagh Andrew anasema Covid-19 haijazuia hitaji la ngono

Bronagh Andrew, meneja wa shughuli za muungano unaohamasisha umma kuelewa biashara harabu ya binadamu (Tara) katika mji wa Glasgow, alisema : “Hii hali ya kuifanya miili ya wanawake kama vyombo na bidhaa kwa ajili ya mapato ya kifedha inasababisha kutokuwepo kwa usawa wa jinsia ya kike na madhara mengine mengi kwa wanawake waathiriwa.

“Covid-19 haikuzuia hitaji la ngono kwa wanaume. Jambo pekee litakalozuia ni kuchukuliwa kwa hatua kabambe dhidi ya wale wanaoamua kulipia ngono na wale wanaonufaika na madhara wakati sote tunahangaika kupata usawa wa kijinsia

“Katika kipindi chote cha janga, Tara imeendelea kutoa makazi salama, usaidizi wa kifedha, huduma za afya, ushauri wa kisheria, na utetezi usaidizi wa kihisia kwa wanawake wanaohitaji huduma hizo, wakati wakiendelea kupona majeraha ya uzoefu walioupitia katika biashara ya ngono.

Operesheni ya pamoja

Hivi karibuni uchunguzi uliofanywa na polisi ya Scotland ulibaini maelfu ya pauni yaliyohamishwa baina ya akaunti za benki mbalimbali.

Operesheni hiyo iliyolenga utumiwaji vibaya wa kingono umefanyika Scotland mwaka huu, huku Glasgow ikiongoza kwa idadi ya wahalifu waliokamatwa ambao walikuwa 13 na waathiriwa walikuwa 25.

Operesheni ya pamoja ya maafisa kutoka Scotland na Romania iliwezesha kukamatwa kwa wafanyabiashara haramu ya wanawake 24 , 10 nchini Uingereza na 14 nchini Romania.

Mwaka 2019, watu wanne walifungwa jela kwa kipindi cha miaka 36 kwakuwasafirisha na kuwauza kingono waathiriwa 10 na kuwalazimisha kuolewa kwa muda katika Scotland.

Muathiriwa mmoja aliuzwa katika mtaa wa katikati mwa jiji la Glasgow kwa takriban pauni 10,000.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *