img

Kiboko: ‘Kilichokamatwa ni chenga za mkaa sio dawa za kulevya’

December 1, 2020

MFANYABIASHARA Ayubu Kiboko amedai mahakamani kwamba kilichokamatwa nyumbani kwake ni chenga chenga za mkaa sio chenga zinazosadikiwa kuwa dawa za kulevya.

Kiboko ameiomba Mahakama Kuu Kitengo cha Rushwa na Uhujumu Uchumi imwachie huru na amekana tuhuma kujihusisha na biashara haramu ya dawa.

Kiboko amedai hayo leo wakati akijitetea kwa kuongozwa na Wakili Majura Magafu mbele ya Jaji Lilian Mashaka.

Kibiko alikana vielelezo vivyotolewa na upande wa Jamhuri ambavyo ni chenga au unga uliokuwa katika mfuko wa nailoni angavu, vikopo viwili vyenye unga mweupe, mfuko mweusi wenye unga mweupe ndani na mfuko unaodaiwa kukutwa kwenye eneo la kutunzia viatu ambapo alidai kuwa vyote hivyo hakuwahi kuviona zaidi ya kuviona mahakamani na siku hiyo hakukufanyika upekuzi katika eneo la kutunzia viatu.

Kiboko amemaliza kujitetea bado mkewe Pili ambaye anatarajiwa kuanza utetezi wake.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *